Zifahamu sumu zinatumiwa na majasusi kuua watu

Sergei and Yulia Skripal?

Chanzo cha picha, FACEBOOK

Maelezo ya picha,

Jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na Binti yake Yulia waliauawa kwa sumu hatari wakiwa London mwaka wa 2018

Mnamo agosti tarehe 20 mwaka wa 2020, kiongozi wa Upinzani wa Urusi na mwanaharakati wa kupambana na ufisadi Alexei Navalny aliwekeea sumu ya kulemaza neva kwa jina Novichok na kukimbizwa akiwa hospitalini katika hali mbaya .

Uchunguzi ulionyesha kupatikana kwa smu hiyo katika damu yake na hilo likazua hofu kwamba bado kuna matumizi ya sumu kama silaha na hasa kuwaua watu .

Kunazo serikali zinazoshtumia kwa kuwalenga wapinzani wake kutumia silaha kama sumu hiyo.Ongezeko la mauaji ya kutumia sumu linazua hamu ya watu wengi kuzijua sumu hizo na jinsi zinavyotumiwa kama silaha ya kuua ama kulemaza . Hizi hapa aina tano ya sumu hatari zinazotumiwa kama silaha ya kuua

Polonium 210

Majasusi wa Urusi walitumia kemikali yenye mionzi kumtilia sumu jasusi wa zamani wa FSB Alexander Litvinenko huko London mnamo 2006, walisema wachunguzi wa Uingereza. Wenzake wa zamani wa ujasusi wa Urusi waliripotiwa kumwaga sumu hiyo kwenye chai yake. Siku 23 zilipita kati ya siku alipolazwa hospitalini na kifo chake.

Polonium 210 haiwezi kununuliwa sokoni na haiwezekani kugundua ikiwa uchunguzi utaanza kuchelewa. Inaweza kuishi kwa siku 138. Kwa asili, inaonekana tu kwa idadi ndogo kama bidhaa ya kuoza ya mionzi.

Chanzo cha picha, SIMONOVSKY DISTRICT COURT/HANDOUT VIA REUTERS

Nchi zenye nguvu za nyuklia ulimwenguni ndizo pekee ambazo zinaweza kutoa poloniamu kwa idadi ambayo inaweza kutumika kuua. Ili kutoa kipimo hatari cha nanogramu 100, mtu atahitaji kilo mia kadhaa za madini ghafi ya uranium. Katika mtambo wa nyuklia, mtu anaweza kutengeneza poloniamu kwa kuunda mseto wa bismuth na nyutroni.

Kuishika poloniamu, hata hivyo, sio hatari sana. Wakati imefungwa vizuri katika pakiti ni salama. Mionzi haitapenya hata karatasi.

Walakini, ikiwa imevutwa kwa pumzi au au imfikie mtu tumboni , huharibu leukocytes katika damu na husababisha upungufu wa damu. Pia huharibu seli za shina na kuzizuia kujizalisha . Waathiriwa hufa ndani ya siku chache au wiki.

Ricin

Ricin ni moja ya sumu hatari zaidi ulimwenguni. Miligramu chache tu za protini hii zinaosha kuua mtu wakati wa kudungwa sindano, kumezwa au kuvuta kwa pumzi. Inaweza kutolewa kutoka kwa mbegu za mmea wa mafuta ya castor Ricinus communis.

Ikiwa ndani ya mwili, ricin huzuia utengenezaji wa protini muhimu. Kama matokeo, mfumo mkuu wa neva, figo, ini na viungo vingine vitashindwa kufanya kazi . Kifo kwa kufeli kwa viungo vingi au mshtuko wa moyo na mishipa kitatokea ndani ya siku chache.

Ricin alijulikana katika kesi ya mauaji ya Georgi Markov. Jasusi wa kikomunisti wa Kibulgaria alifyatua risasi ndogo na yenye sumu hiyo kwenye mguu wake mnamo 1978 huko London; Markov alikufa siku tatu baadaye.

Wachunguzi wakati huo walipendekeza kwamba shirika la KGB la Soviet linaweza kuwa limetoa sumu hiyo.

Imedaiwa kwamba dikteta wa Bulgaria Todor Zhivkov aliamuru kuuawa kwa mwandishi huyo , kwa sababu Markov alichapisha maelezo makali juu ya wandani wa utawala wa kikomunisti. Matangazo yake ya kejeli kwenye vyombo vya habari vya magharibizikiwemo BBC, RFE na DW, yalikuwa maarufu kwa wasikilizaji huko Bulgaria.

Chanzo cha picha, TOSHIFUMI KITAMURA

VX

Hivi karibuni, mnamo Februari 13, 2017, wanawake wawili walimnyunyizia usoni kemikali ya kupoza neva VX Kim Jong Nam, ambaye ni kakake wa kambo kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un. Mauaji hayo yalifanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur. Kim Jong Nam alikufa njiani akipelekwa hospitali nyingine muda mfupi baada ya shambulio hilo.

Wanawake hao wawili walikuwa kutoka Vietnam na Indonesia na wanadai kwamba hawakujua kuwa dawa hiyo ilikuwa kemikali ya kupooza neva na kwamba walifanywa kuamini kwamba walikuwa sehemu ya maigizo ya runinga . Wachunguzi wanaamini kwamba Kim Jong Un aliamuru mauaji hayo.

VX ni sumu hatari zaidi ya kemikali inayojulikana. Miligramu 0.4 tu ya sumu hii inatosha kuua mtu mzima.

Mwanakemia Ranajit Gosh aligundua sumu hii mnamo miaka ya 1950 wakati akitafiti juu ya dawa za wadudu katika maabara ya Viwanda vya Kikemikali vya Uingereza

Kemikali hiyo imepigwa marufuku chini ya Mkataba wa Silaha za Kemikali wa 1997. Korea Kaskazini shaijatia sahihi mkataba huo

Matukio mengine ya kihistoria ambayo VX ilitumika ni pamoja na mauaji ya watu mwaka wa 1988 ambapo takriban raia 5,000 wa Kikurdi waliuawa na vikosi vya dikteta wa Iraqi Saddam Hussein katika mji wa Halabja. Na mwanzoni mwa miaka ya 1990 kiongozi wa dhehebu la Kijapani Shako Asahara alitengeneza VX na kumuua mtu mmoja .

Botox

Sumu hii iliyotengenezwa na Clostridium Botulinum, inajulikana sana kwa matumizi ya mapambo. Walakini, sumu ya botulism ndio ile ile inayohusika na sumu ya chakula. Bakteria hiyo iko kila mahali, lakini inaweza kukuzwa na kuongezeka tu katika mazingira bila oksijeni. Botox ni sawa na sumu inayofanya kazi katika maambukizo ya pepopunda.

Ni protini ya neva, ambayo inazuia usafirishaji wa ishara na seli za neva. Hii inasababisha kupooza kwa mfumo wa neva wa mimea na udhaifu wa misuli. Microgramu 0.3 tu za Botox zinaweza kuwa mbaya.

Chanzo cha picha, Getty Images

Botox inachukuliwa kuwa silaha ya kibaolojia. Wasiwasi mkubwa ni kwamba inaweza kutumika katika kutekeleza ugaidi wa silaha za kemikali. Iraq chini ya Saddam Hussein ilikuwa na mpango wa kutengeneza Botox kama silaha ya vita.

Mkuu wa shirika la ujasusi Fabian Escalante, wakati mmoja alisema CIA au wahamiaji wa Cuba wakati mmoja walikuwa wamepanga kumuua Fidel Castro na sigara iliyowekwa Botox. Hata hivyo kuwepo kwa njama kama hiyo hakuwezi kuthibitishwa kwa njia huru

Chanzo cha picha, Reuters

BTX

Batrachotixin ni sumu nyingine ya neva yenye nguvu sana. Sumu hii huzalishwa kutoka kwa vyura wenye sumu kali, spishi iliyo hatarini huko Amerika Kusini. Gramu 0.2 tu zinatosha kumuua mwanadamu. Sumu hiyo husababisha misuli ya moyo kuganda na kusababisha kupatwa na mshtuko wa moyo .

Haiwezekani kuweka vyura wenye sumu kali katika na kisha kutoa sumu hiyo, hata hivyo. Ni katika makazi yao ya asili katika misitu ya Amerika ya Kati na Kusini ndio wanyama wanaweza kutoa sumu hiyo. Inaaminika kwamba vyura hao wanaweza kukuza tu sumu kama matokeo ya kumeng'enya mende na wadudu fulani.

Maelfu ya vyura watahitajika kutoa BTX ya kutosha kuua mwanadamu. Walakini, hakuna kesi zinazojulikana za sumu ya binadamu na BTX.