Tetesi za soka Ulaya Jumapili 01.08.2021: Harry Kane, Martinez, Grealish, Saul, Romero, Cantwell, Locatelli

Nahodha wa England Harry Kane

Chanzo cha picha, Getty Images

Nahodha wa England Harry Kane ataiambia Tottehnam kwamba anataka kujiunga na Manchester City wakati mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atakapofanya mazungumzo na klabu hiyo wiki ijayo. (Telegraph - subscription required)

Aston Villa iko tayari kukubali dau la Manchester City la £100m kumnunua kiungo wa kati wa England Jack Grealish, 25. (Sky Sports)

Kikosi hicho cha mkufunzi Dean Smith pia kitawasilisha ombi la kumnunua kiungo wa kati wa Norwich na England Todd Cantwell, 23, iwapo Grealish ataondoka Villa Park. (Express)

Villa pia inatarajiwa kuwasilisha ombi la pili la kumsaini kiungo wa kati wa Southampton James Ward Prowse baada ya dau la £25m kumnunua mchezaji huyo kukataliwa (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal inafikiria kumtumia beki wa Uhispania mwenye umri wa miaka 26 Hector Bellerin kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez , 23 huku klabu ya Tottenham pia ikiwa mbioni kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Argentina iwapo watafanikiwa kumuuza Harry Kane 28. (Athletic - subscription required)

Manchester United ina matumaini ya kutaka kumsaini mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Haaland, 21, msimu ujao na wanaamini kwamba uhusiano wake na kocha Ole Gunnar Solskjaer huenda ukachangia kwa kuwa mchezaji huyo ni raia wa Norway sawa na kocha huyo. (Star)

Chelsea inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Atalanta, Bayer Leverkusen na Borussia Dortmund kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na klabu ya St. Etienne Lucas Gourna-Douath, ambaye atakuwa na umri wa miaka 18 kufikia wiki ijayo. (RMC Sport - in French)

Wawakilishi wa kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Uhispania Saul Niguez wataelekea England siku ya Jumatatu ili kujadiliana kuhusu kuhamia katika ligi ya Premia , huku klabu za Manchester United na Liverpool zikimtafuta mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United inajianda kumpatia Luke Shaw kandarasi mpya baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuonesha mchezo mzuri akiichezea England katika michuano ya Euro 2020. (Mail)

Juhudi za klabu ya Tottenham kutaka kumsajili beki wa Argentina mwenye umri wa miaka 23 Cristian Romero kutoka Atalanta zimegonga mwamba baada ya awamu ya mwisho ya mazungumzo kati ya klabu hizo mbili kukamilika bila makubaliano. (Gianluca Di Marzio - in Italian)

Beki wa Manchester City John Stones, 27, anakaribia kupatiwa kandarasi mpya , lakini mazungumzo ya kumuongezea kandarasi mpya winga wa England Raheem Sterling yamegonga mwamba. (Mirror)

Fenerbahce inafikiria kumsaini beki wa Portugal na Arsenal Cedric Soares, 29. (Fotomac - in Turkish)

Crystal Palace inafikiria kumsaini winga wa Arsenal Reiss Nelson, 21, kwa mkopo. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Juventus inatatizika kuafikia dau la pauni milioni 34 la Sassuolo kumnunua mchezaji wa Itali mwenye umri wa miaka 23 Manuel Locatelli, huku Liverpool na Arsenal zikiwa tayari kumsajili kiungo huyo.. (Sky Sport Italia via Mail)

Everton na Arsenal zinamchunguza mshambuliaji wa klabu ya Schalke Matthew Hoppe 23, ambaye anaichezea Marekani katika kombe la Gold Cup. (Journalist Grant Wahl via Sun)

Fulham ipo katika mazungumzo na klabu ya Flamengo kuhusu makubaliano ya dau la £6.8m ili kumnunua mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 20 Rodrigo Muniz. (Mail)