F-35: Fahamu kwanini ndege hii ya kivita ya Marekani ni bora kuliko nyengine zote

Ndege ya F-35 ilichukua zaidi ya miaka 15 kuundwa Marekani

Chanzo cha picha, LOCKHEED MARTIN

Maelezo ya picha,

Ndege ya F-35 ilichukua zaidi ya miaka 15 kuundwa Marekani

Wakati utawala wa rais Bill Clinton ulipotoa wazo la ndege ya kivita yenye 'majukumu mawili tofauti' 1995 , ndio iliokuwa suluhu kwa changamoto chungu nzima za kijeshi.

Lengo lilikua kutengeneza ndege ya kijeshi ilio na teknolojia ya kisasa ili kuweza kutekeleza operesheni tofauti kwa vitengo vitatu vya jeshi vya Marekani.

Jeshi la wanaanga wangeitumia ndege hiyo kama mbadala wa ndege ya kivita ya F-16 katika mashambulizi ya angani , kushambulia maeneo ya ardhini na kutoa usaidizi kwa wanaanga hewani.

Jeshi la wanamaji lingeitumia kuimarisha mashambulizi ya meli inayobeba ndege za kivitaNa kila mtu ikiwemo washirika wake , wangeitumia kukusanya ujesusi ambo ungesambazwa kwa washirika katika vita vya siku zijazo.

Mara ya kwanza kuna wale waliodhania kwamba ndege hiyo ya kivita ilikuwa ndoto ambayo haingetimia - mradi uliotarajia mambo mengi kutoka kwa ndege moja na kwamba usingefanikiwa kutokana na gharama zake.

Mradi huo usingeanza iwapo vitisho vya kijeshi vingekuwa vingi , lakini wakati huo muungano wa Usovieti ulikuwa umeanguka na mapato ya China yalikuwa asilimia 3, hivyobasi utawala wa rais Clinton ukaamua kuchukua hatua hiyo.

Kwa sasa mamia ya ndege aina ya f-35 zinafanya kazi katika majeshi zaidi ya 10 duniani.

Ilichukua muda mrefu kufanikiwa kuliko ilivyopangwa hapo awali, lakini mwishowe ndege hiyo ilikidhi malengo yake ya kuishi .

Hiyo inaifanya kuwa moja wapo ya ndege iliotengenezwa kwa ustadi mkubwa wa uhandisi wa kizazi cha baada ya vita baridi - kwa kweli ndege hiyo ni ushahidi wa nidhamu na ustadi wa tasnia ya anga ya Marekani.

Hatahivyo, hujafuatilia mpango wa F-35 kwa karibu, pengine hujui zaidi ya haya.

Rais Trump aliingia madarakani akiwa na uelewa mdogo juu ya F-35, na polepole alikuja kuelewa ni kwanini ilikuwa muhimu sana katika jeshi la pamoja.

Lakini ni nini haswa kinachoifanya ndege ya F-35 kuwa ya kipekee duniani?

Haionekani na maadui. Wakati ndege ya F-35 inaposhiriki katika mazoezi, kawaida huzishinda ndege za adui kwa kiwango cha 20 kwa 1.

Ingefanya vivyo hivyo wakati wa vita dhidi ya wanajeshi wa Urusi au Wachina, kwa sababu iliundwa kunyonya au kupotosha nishati ya rada, kwa hivyo marubani wa ndege za adui hawawezi kuiona kabla haijashambulia.

Kwa kuongezea, F-35 ina mfumo wa hali ya juu ambao unadanganya au kukandamiza rada za adui, angani na ardhini.

Rada hizo zinaweza kugundua kitu kwa mbali, lakini haziwezi kuifuatilia au kuishambulia F-35.

Pia, injini ya ndege hiyo ina uwezo wa kupunguza joto kabla ya makombora yanayotafuta joto kuishambulia.

Ni zaidi ya ndege ya kivita . F-35 sio tu ndege ya kupambana bali pia ni ndege inayoweza kuishi muda mrefu kuwahi kuundwa.

Katika jukumu lake, ina uwezo wa kusafisha anga za ndege za maadui ambazo zinatishia majeshi ya Marekani.

Chanzo cha picha, AFP

Vilevile inaweza kushambulia na kuangamiza maeneo yanayolengwa ardhini, au baharini kwa kutumia mabomu na makombora tofauti..

Sensa zake

Lakini huo ni mwanzo tu. Sensa za ndani za F-35 zinaweza kukusanya na kusambaza habari za ujasusi katika maeneo mbalimbali.

Mfumo wake wa kuweza kuzuia mifumo ya ndege nyengine pamoja na vifaa vyake vya mashambulizi angani inaifanya ndege hiyo kuwa bora dhidi ya ndege nyengine za kivita.

Uwezo wake wa kupaa angani wima na kuweza kutua mahali popote ambapo wanamaji watataka huku ikiwa na uwezo wa kubeba silaha za nyuklia ili kutoa ulinzi.