Afghanistan: Taliban yazidi na mashambulizi huku ikionya Marekani dhidi ya kuingilia kati

ta

Chanzo cha picha, Reuters

Taliban wameteka miji mikuu mitatu ya mikoa nchini Afghanistan wakati wanaendelea kupata mafanikio makubwa katika ya kuchukua maeneo mengi ya nchi .

Walichukua udhibiti wa mji muhimu wa kaskazini wa Kunduz Jumapili, na vile vile Sar-e-Pul na Taloqan.

Inamaanisha miji mikuu mitano ya mikoa sasa ipo mikononi mwa wanamgambo tangu Ijumaa, na Kunduz ikiwa ndio mafanikio yao makubwa mwaka huu .

Taliban walisema hakuna makubaliano juu ya kusitisha mapigano na serikali.

Msemaji wa kikundi hicho alionya dhidi ya uingiliaji wowote wa Marekani nchini Afghanistan wakati akizungumza na runinga ya Al Jazeera siku ya Jumapili.

Chanzo cha picha, Reuters

Vurugu zimezidi kote Afghanistan baada ya majeshi ya Marekani na vikosi vingine vya kimataifa kuanza kuondoa wanajeshi wao nchini, kufuatia miaka 20 ya operesheni za kijeshi.

Wapiganaji wa Taliban wamepiga hatua za haraka katika wiki za hivi karibuni. Baada ya kukamata maeneo makubwa ya mashambani, sasa wanalenga muhimu ya taifa hilo

Miji mitatu ya kaskazini iliangukia udhibiti wa Taliban ndani ya masaa machache baada ya kila mji kutekwa Jumapili, na mkazi mmoja huko Kunduz akielezea hali hiyo kama "machafuko makubwa ".

Serikali ya Afghanistan, wakati huo huo, ilisema vikosi vyake vinapigania kuchukua maeneo yenye miundo mbinu muhimu.

Mapigano makali pia yameripotiwa huko Herat magharibi, na katika miji ya kusini ya Kandahar na Lashkar Gah.

Maelfu ya raia wamehama makazi yao mwaka huu.

Familia, ikiwa ni pamoja na watoto wachanga na wadogo, wamekuwa wakipata hifadhi katika shule ya mji wa Asadabad kaskazini mashariki.

"Mabomu mengi yalirushwa katika kijiji chetu. Taliban walikuja na kuharibu kila kitu. Tulikuwa hatuna usaidizi na tulilazimika kutoroka katika nyumba zetu. Watoto wetu na sisi wenyewe tunalala chini katika hali mbaya", Gul Naaz aliambia AFP.

"Kulikuwa na kurushwa kwa risasi, mmoja wa binti zangu wa miaka saba alitoka nje wakati wa mapigano hayo na kutoweka. Sijui ikiwa yuko hai au amefariki dunia", mkazi mwingine aliyetoroka makazi yake amesema.

Marekani imeongeza mashambulio yake ya anga katika ngome za Taliban, na maafisa wa jeshi la Afghanistan wanasema wanamgambo wameuawa.

Kwa upande wao, Taliban wanasema mashambulio ya angani yalitokea katika hospitali mbili na shule katika mji wa Lashkar Gah.

Hakuna kati ya madai hayo yamethibitishwa.

Ubalozi wa Marekani nchini Afghanistan umeshutumu "shambulio jipya kali la Taliban dhidi ya miji ya Afghanistan", ukisema hatua za kundi hilo unalazimisha utawala wake na haikubaliki.

"Wanaonyesha kupuuza ustawi na haki za raia na hilo litazidisha mzozo wa kibinadamu nchini humo", ilisema katika taarifa.

Umuhimu wa Kunduz

Kutwaliwa kwa eneo la Kunduz ni kwenye umuhimu mkubwa kwa Taliban tangu walipoanzisha mashambulizi yao mnamo mwezi Mei.

Mji huo, nyumbani kwa watu 270,000, unachukuliwa kuwa lango la utajiri wa madini katika mikoa ya kaskazini.

Na eneo lake hufanya liwe muhimu kimkakati kwani kuna barabara kuu zinazounganisha Kunduz na miji mingine mikubwa, pamoja na Kabul, na jimbo linashirikishana mpaka na Tajikistan.

Chanzo cha picha, EPA

Mpaka huo unatumika kwa usafirishaji haramu wa dawa za kulevya aina ya kasumba na heroine kutoka Afghanistan kwenda Asia ya Kati, ambazo husafirishwa hadi Ulaya.

Kudhibiti eneo la Kunduz kunamaanisha kudhibiti moja ya njia muhimu zaidi za kusafirisha dawa za kulevya katika eneo hilo.

Pia ni mfano muhimu kwa Taliban kwasababu ilikuwa ngome ya msingi upande wa kaskazini kabla ya mwaka 2001.

Wanamgambo waliteka mji huo mnamo mwaka 2015 na tena mnamo mwaka 2016 lakini hawajawahi kuushikilia kwa muda mrefu.

Je! Afghanistan inaachwa bila marafiki?

Uchambuzi na Paul Adams,

Mwandishi wa Kidiplomasia wa BBC Jenerali wa zamani wa Uingereza Sir Richard Barrons anasema kuna hisia ya hatari nchini Afghanistan "inajihisi isiyo na marafiki" baada ya kushindwa katika vita hivi karibuni na uwezekano wa kujiondoa kwa wanadiplomasia na wanakandarasi kutoka Kabul ikiwa mambo yatazidi kuwa mabaya.

Ni mapema mno kuanza kushuku juu ya kujiondoa kutoka mji mkuu, ikirudia njia ambayo Wamarekani waliondoka haraka Vietnam katika hatua ya mwisho ya vita huko, mnamo mwaka 1975.

Lakini katika siku za hivi karibuni, Waingereza na Marekani wametoa wito kwa raia wao kuondoka nchini humo kwasababu ya tishio la kutokea kwa hatari.

Ni jambo ambalo wapangaji wa jeshi la magharibi wamekuwa na wasiwasi nalo kwa muda, kufuatia uamuzi wa Rais wa Merekani Joe Biden, mnamo Aprili, wa kuondoa vikosi vya Marekani ifikapo tarehe 11 Septemba.

Mnamo mwezi Juni, hati za Wizara ya Ulinzi ya Uingereza zilipatikana katika kituo cha basi cha Canterbury.

Mmoja wao alionyesha wasiwasi huu tu, akizungumzia juu ya hitaji la kukabiliana na 'kutelekezwa' huko Afghanistan.

Kwa maneno mengine, wapangaji walikuwa wanajua tu juu ya kutengengeza hisia ya hatari kwamba Afghanistan inaweza kweli kuachwa "bila marafiki".

Lakini sivyo hali ilivyo.

Mashambulio ya angani yanayotekelezwa na Marekani bado yanatumika katika jaribio la kusitisha uvamizi wa Taliban.

Uingereza na Merekani bila shaka watakuwa na silaha zilizofichwa chini ya ardhini, wakifanya kila namna kumaliza wimbi hili la vita.