Mabadiliko ya hali ya hewa : Ripoti ya Jopo la wanasayansi wa dunia IPCC 'yaonesha ishara ya hatari kwa binadamu '

Chanzo cha picha, EPA
Shughuli za binadamu zinabadili hali ya hewa kwa njia zisizotarajiwa na wakati mwingine zisizoweza kurekebishwa , imesema ripoti kuu ya Umoaja wa Mataifa.
Utafiti wa kihistoria umeonya juu ya kuongezeka kwa mawimbi ya joto, ukame na mafuriko na kuvukwa kwa ukomo wa joto duniani katika kipindi cha muongo mmoja pekee ujao.
Ripoti hiyo iliyoitwa "ni ishara ya hatari kwa binadamu", anasema Mkuu wa Umaja wa Mataifa.
Lakini wanasayansi wanasema janga hilo linaweza kuepukika iwapo dunia itachukua hatua za haraka.
Kuna matumaini kwamba kupunguzwa kwa kiwango kikubwa zaidi cha utoaji wa hewa chafu kunaweza kusaidia kuzuia kuongezeka zaidi kwa viwango vya joto duniani.
Akiunga mkono matokeo ya utafiti ya wanasayansi, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema: "iwapo tutaweka pamoja nguvu , tunaweza kuepuka janga la hali ya hewa.
Lakini hadi leo, ripoti inabainisha wazi, kuwa hakuna muda wa kuchelewa na hakuna muda wa kutoa sababu. Ninawategemea viongozi wa serikali na wadau wote kuhakikisha mafanikio ya COP26 yanafikiwa."
Tathmini ya hali ya hewa ya dunia imefanya jopo la Umoja wa Mataifa la wana mazingira wa serikali mbali mbali (IPCC), na kikundi cha wanasayansi ambao kazi yao iliidhinishwa na serikali za dunia.
Jopo hilo linaongoza msururu wa ripoti ambazo zitachapishwa kwa miezi kadhaa ijayo na ni tathmini kuu ya kwanza ya sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani kuwahi kufanyika tangu mwaka 2013
Kwa kauli thabiti, waraka wa IPCC unasema "bila shaka kwamba ushawishi wa binadamu umechemsha anga, bahari na ardhi".
Matendo ya binadamu yamesababishamabadiliko ya tabia nchi na kufanya dunia kuwa na joto zaidi
Kulingana na Profesa Ed Hawkins, kutoka Chuo Kikuu cha Reading, Uingereza,, ambaye pia ni mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo, wanasayansi hawawezi kuwa wazi zaidi ya ilivyo kwa sasa.
Waandishi wa ripoti wanasema kwamba tangia mwaka 1970, viwango vya joto kwenye sakafu ya dunia vimeongezeka haraka zaidi kuliko ilivyowahi kutokea katika mwaka wa 50 kwa miaka 200 iliyopita.
Iwe ni mawimbi ya joto kama yale yanayoshuhudiwa Ugiriki na magharibi mwa Marekani, au mafuriko kama yale yaliyotokea Ujerumani na Uchina , "shughuli za binadamu zimechangia " kwa zaidi ya muongo uliopita.
Mambo muhimu katika ripoti ya IPCC
- Viwango vya joto la dunia vilikuwa vya juu kwa 1.09C katika muongo wa kati ya 2011-2020 kuliko kati ya 1850-1900.
- Miaka mitano iliyopita kumeshuhudiwa joto la juu zaidi kuwahi kurekodiwa tangu 1850
- Viwango vya hivi karibuni vya maji ya bahari vilipanda kwa karibu mara tatu ikilinganishwa na kati ya mwaka 1901-1971
- Ushawishi wa binadamu "una uwezekano mkubwa " wa kiwango cha (90%) ya sababu kuuza kuyeyuka kwa barafu ya dunia tangu miaka ya1990 na kupungua kwa barafu ya bahari ya Arctic
Ripoti hiyo pia inabainisha wazi kuwa joto tunalolishuhudia leo limesababisha mabadiliko kwa mifumo mingi ya sayari , athari ambazo haziwezi kurekebika kwa kipindi cha karne hadi milenia.
Bahari zitaendelea kuchemka na kuwa na tindikali zaidi. Barafu za vilele vya milima zitendelea kuyeyuka kwa miongo au karne
"Athari zitaendelea kuwa mbaya zaidi kila mara dunia inapochemka ," alisema Profesa Hawkins.
Chanzo cha picha, Justin Sulivan
Jimbo la California linalokabiliwa na ukame limeshuhudia kupungua kwa viwango vya maji katika ziwa Oroville
Inapokuja katika suala la kupanda wa viwango vya maji ya bahari , wanasayansi wameelezea kuwa uwezekano wa ongezeko la viwango tofauti vya maji umesababishwa na utoaji wa hewa chafu.
Hatahivyo, ongezeko la karibu mita kimo cha maji cha 2 mwishoni mwa karne hii haliwezi kupuuzwa- na ongezeko la mita 5 linaweza kuwepo kufikia mwaka 2050
Huku matokeo ya aina hii huenda yasiwe tisho kwa dunia, , yanaweza kutishia maisha ya mamilioni zaidi ya watu wanaoishi maeneo ya mwambao pamoja na mafurika ifikiapo mwaka 2100.
Chanzo cha picha, ANDY RAIN
Waandamanaji wanataka viongozi kuchukua hatua dhidi ya mabdiliko ya tabia nchi
Takriban kila taifa duniani lilisaini malengo ya makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa mwaka 2015.
Makubaliano haya yalilenga kuendelea kuviweka viwango vya joto la dunia chini ya nyuzi joto 2 na kujaribu kufanya juhudi za kuiweka chini ya nyuzi joto 1.5. ( 1.5C).
Athari za kwenda zaidi ya nyuzi joto 1.5 kwa kipindi cha miaka kadhaa ni kitu ambacho hakitapendwa katika dunia ambayo tayari imekwisha shuhudia matukio mabaya ya majanga huku viwango vya joto vikiongezeka tangu kabla ya enzi ya viwanda kwa kiwango cha nyuzijoto 1.1
"Tutashuhudia hata mawimbi mazito na ya mara kwa mara ya joto ," alisema Dkt Friederike Otto, kutoka Chuo kikuu cha oxford, nchini Uingereza, na ambaye ni mmoja wa waandishi wa ripoti ya IPCC.
Je nini kinaweza kufanyika?
Huku ripoti hii ikiwa wazi zaidi athari za joto, wanasayansi wana matumaini zaidi kwamba iwapo tutaweza kupunguza hewa chafu kwa nusu ifikapo mwaka 2030 na kufikia kiwango cha sifuri katikati ya karne hii, tunaweza kuzuia na huenda kurejesha nyuma viwango vya joto la dunia.
Ripoti hii inasema kulingana na matukio ya utoaji wa hewa chafu uliotathminiwa na wanasayansi, malengo yote ya Paris yatakuwa yamekiukwa , katika karne hii iwapo hewa chafu ya kaboni haitapunguzwa.
Ili kufikia kiwango cha sifuri hewa chafu inapaswa kupunguzwa sana kwa kutumia teknolojia safi, na kuachana kabisa na utumiaji wa hewa ya kaboni na hifadhi yake, au kuimaliza kwa kupanda miti.
"Awali wazo lilikuwa ni kuwa tunaweza kuongeza viwango vya joto hata baada ya kufikia kiwango kamili cha sifuri ," anasema mwandishi mwenza wa ripoti, Profesa Piers Forster kutoka Chuo kikuu cha f Leeds, Uingereza.
Athari tano zijazo
• Viwango vya joto vitafikia nyuzi joto 1.5 juu ya vile vya kati ya 1850-1900 ifikapo mwaka 2040 kwa kuzingatia aina zote za uchafuzi wa hali ya hewa
• Bahari ya Arctica itakuwa na uwezekano wa kutokuwa na barafu ifikapo mwezi Septemba walau mara moja kabla ya 2050
• Kutakuwa na ongezeko la matukio mabaya zaidi "yasiyotarajiwa katika rekodi ya historia " hata katika nyuzi joto 1.5
• Matukio ya kuongezeka kwa viwango vya juu zaidi vya maji ambavyo hutokea mara moja kwa karne katika siku chache zilizopita yanakadiriwa kutokea walau kila mwaka kufikia mwaka 2100
• Kutakuwa na uwezekano wa kuongezeka kwa hewa ya moto katika maeneo mengi
Huku makadirio yakionesha ongezeko la viwango vya joto wazi zaidi kuliko wakati wowote ule katika ripoti hii, na athari nyingi haziwezi kuepukika, waandishi wa ripoti hii wametahadharisha dhidi ya athari hizo kusababisha vifo.
Kwa viongozi wa kisiasa, ripoti hii ni mistari mingine mirefu ya miito ya tahadhari , lakini kwasababu imekuja karibu sana na kikao cha dunia cha COP26 cha mabadiliko ya hali ya hewa cha Novemba , inabeba uzito wa ziada.