Dira ya Dunia 09/08/2021: Rais Samia azungumzia kuhusu Mashtaka ya Mbowe, katiba mpya na uongozi wake

Dira ya Dunia 09/08/2021: Rais Samia azungumzia kuhusu Mashtaka ya Mbowe, katiba mpya na uongozi wake

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Salim Kikeke, Rais Samia amesema ana imani sheria itachukua mkondo wake.

Wafuasi wa Bwana Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa.

Aidha katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha.