Mahojiano Maalum na Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe hayajachochewa kisiasa

Mahojiano Maalum na Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe hayajachochewa kisiasa

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Salim Kikeke, Rais Samia amesema ana imani sheria itachukua mkondo wake.

Wafuasi wa Bwana Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa.

Aidha katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha.

Mahojiano hayo kwa urefu zaidi usikose matangazo ya Dira ya Dunia ya redio saa kumi na mbili unusu jioni, matangazo ya Dira ya Dunia ya televisheni saa tatu kamili usiku kupitia Star Tv na fuatilia mitandao yetu ya kijamii, Facebook, Instagram na Youtube.