Mahojiano Maalum na Rais Samia: Tuko hapa kuonyesha kuwa wanawake pia wanaweza kuongoza

SSH

Rais wa Tanzania amesema kuna watu ambao walitilia shaka kuwa alikuwa na sifa ya kuongoza wakati alipochukua hatamu kwa sababu ni mwanamke.

Wengine "hawaamini kuwa wanawake wanaweza kuwa marais bora na tuko hapa kuwaonyesha," Samia Suluhu Hassan aliambia BBC.

Mnamo Machi, Samia mwenye umri wa miaka 61 aliapishwa baada ya mtangulizi wake kufariki ofisini.

Hivi sasa ndiye mwanamke pekee wa kike anayeongoza nchi . Urais wa Ethiopia ni jukumu la kiitifaki bali sio wadhifa ulio na mamlaka .

Maelezo ya video,

Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe hayajachochewa kisiasa

"Hata wafanyikazi wangu wengine wa serikali walinipuuza kama mwanamke, lakini hivi karibuni wamekubali uongozi wangu," Bi Samia alisema.

"Lakini hii sio tu Afrika, hata Marekani, [Hillary] Clinton alifika mahali ambapo tulifikiri angekuwa rais lakini hakuweza," akaongeza.

Bi Samia, ambaye alipandishwa cheo kutoka kwa makamu wa rais, alishauri kuwa kuangazia kutekeleza mipango ya maendeleo na kutanguliza mahitaji ya watu ndiyo njia bora ya kushughulikia wakosoaji.

Aliongeza kuwa licha ya changamoto, nchi zingine zinaweza kujifunza kutoka Liberia na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo zimekuwa na viongozi wa kike.

Rais Samia alichukua nafasi ya John Magufuli ambaye alikufa kutokana na shida ya moyo, alitangaza wakati huo.

Magufuli alishtakiwa kwa kukandamiza wapinzani na kupunguza uhuru mbali mbali . Mrithi wake alionekana kama mtu ambaye ataleta taswira tofauti ya uongozi.

Lakini kukamatwa kwa kiongozi mkuu wa upinzani Freeman Mbowe kwa tuhuma zinazohusiana na ugaidi, kumesababisha wengine kujiuliza ikiwa Rais Samia anaendelea na sera za mtangulizi wake.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Freeman Mbowe alikuwa mkosoaji wa Rais wa zamani wa Tanzania John Magufuli

Hata hivyo, kiongozi huyo wa Tanzania alitetea hatua hiyo akisema mashtaka ya Bw Mbowe "hayakuwa ya kisiasa" kwa sababu alikuwa akichunguzwa tangu Septemba mwaka jana.

"Alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu. Sijui kwa nini alikimbia lakini aliporudi alianza kutish maandamano na madai ya katiba'

"Ninashuku kwamba, kwa kujua mashtaka aliyokuwa akikabiliwa nayo, alihesabu kuwa ikiwa angekamatwa anaweza kudai kuwa ni kwa sababu alikuwa akishinikiza katiba mpya," rais alisema.

Bwana Mbowe alizuiliwa baada ya kusema uchaguzi uliopita ulikumbwa na ulaghai

Rais Samia alisema "ataachia korti kuamua ikiwa ana hatia au hana hatia.

Kiongozi huyo wa Tanzania pia alisema yuko tayari kukutana na wanachama wa upinzani na wadau wengine kujadili mabadiliko ya katiba "wakati ufaao " lakini hakueleza wakati hilo litatokea.

Wakosoaji wanasema katiba ya nchi hiyo inapendelea Chama Cha Mapinduzi kinachotawla nchi hiyo .

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Rais Samia alibadilisha sera ya Tanzania ya kutilia shauku hatari ya ugonjwa wa Covid 19

Rais huyo amechukua mkondo tofauti juu ya janga la Covid 19 kuliko Magufuli, ambaye alipuuzilia makali ya ugonjwa huo .

Bi Samia alisema kuwa kulikuwa na kampeni inayoendelea ya umma ya kuwahamasiaha watu kuchanjwa. Rais alisema kwamba aliamua kupata chanjo hiyo hadharani ili kuwahakikishia wale ambao walikuwa na wasiwasi juu ya usalama wake.

"Lakini wasiwasi wangu mkubwa sasa sio kusita kwa watu kuchanjwa lakini kupatikana kwa chanjo, tumepokea misaada kutoka Marekani na tumepata zingine kutoka kwa mpango wa Covax, lakini hivi karibuni zitakwisha," Bi Samia aliambia BBC.

Mabadiliko ya sera yamepokelewa vyema na kwa sababu mtangulizi wake alizua shaka juu ya kuwapo kwa janga hilo na hatua zilizochukulia kujikinga kama vile kuzuia watu kukaribiana na kuvalia barakoa Badala yake aliwauliza watu wasali na watumie wafukize dawa za asili .

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Watanzania wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kukosoa sera za serikali

Rais Samia pia alitetea serikali yake kwa madai kwamba ameendelea kutekeleza sheria zinaobana uhuru wa vyombo vya habari.

Alisema waandishi wa habari "walikuwa huru kufanya kazi maadamu wanafuata sheria za nchi".

Alisema pia kuwa anasikiliza ukosoaji dhidi yake kwenye mitandao ya kijamii na wanachama wa upinzani na wanaharakati na kuongeza kuwa amezoea, lakini "inatusaidia kujua watu wanafikiria nini, ikiwa tutaipiga marufuku hatutakuwa na jukwaa hilo".