Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 10.08.2021:Messi, Lukaku, Pogba, Doku, Abraham, Lingard, Sterling

Paul Pogba

Chanzo cha picha, EPA

Klabu hiyo ya Ufaransa pia imesitisha jithada zao kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28. (Le Parisien - in French)

Huenda Manchester United inaandaa ofa ya kumjaribu mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Lionel Messi, 34, asihamie Paris St-Germain. (Daily Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

PSG wako tayari kuuza hadi wachezaji 10, pamoja na kiungo wa zamani wa Senegal Idrissa Gueye, 31, ili kukamilisha usajili wa gwiji huyo wa Argentina. (Athletic)

Chanzo cha picha, Getty Images

Baada ya kupitia sehemu ya kwanza ya matibabu yake huko Chelsea, mshambuliaji wa Ubelgiji wa Inter Milan Romelu Lukaku, 28, anaweza kucheza kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi ya premia dhidi ya Crystal Palace Jumamosi. (Daily Star)

Lyon wameweka ofa kupata huduma za mshambuliaji wa Liverpool na Uswizi Xherdan Shaqiri, 29. . (L'Equipe - via Get French Football News)

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United iko tayari kuthibitisha kusainiwa kwa beki wa Real Madrid Raphael Varane, 28, Jumatano - kwa wakati ili Mfaransa huyo kucheza kwenye mchezo wa Ligi ya Premia Jumamosi dhidi ya Leeds. (Daily Star)

Liverpool inaangalia uhamisho wa winga wa Rennes na Ubelgiji Jeremy Doku, 19. (Voetbal 24 - in Dutch)

Mshambuliaji wa Chelsea England Tammy Abraham, 23, analengwa na Arsenal, Roma na Atalanta. (Goal)

Meneja wa Roma Jose Mourinho bado ana hamu ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexander Lacazette, 30. (Gazzetta dello Sport - via Boot Room)

Leicester inataka kumsajili kiungo wa Manchester United Jesse Lingard, 28, ikiwa Mwingereza mwenzake James Maddison, 24, ataondoka klabuni humo. (Football London)

The Foxes pia inasemekana inamtaka beki wa kati wa Uturuki mwenye umri wa miaka 21 wa Schalke Ozan Kabak - ambaye alihudumu sehemu ya mwisho ya msimu uliopita kwa mkopo Liverpool - na mlinzi wa West Ham Mfaransa Issa Diop, 24(Leicester Mercury)

Everton inavutiwa na kiungo wa Uingereza wa Newcastle United Sean Longstaff, 23. (Athletic)

Chanzo cha picha, Getty Images

Bayern Munich wanafikiria kumsaini tena Franck Ribery. Winga huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 38 amekuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo tangu aondoke Fiorentina. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Winga wa Manchester City England Raheem Sterling, 26, anatarajiwa kushiriki mazungumzo ya mkataba mpya na kilabu hiyo. (Sun)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Ufaransa Tanguy Ndombele, 24, anafikiria kuhusu mustakabali wake katika Spurs. (Athletic)