Jinsi Taliban walivyoteka taifa zima la Afghanistan ndani ya siku 10 Pekee

Taliban fighters stand guard in a vehicle along the roadside in Kabul on 16 August.

Chanzo cha picha, Getty Images

Taliban walivamia maeneo yote ya Afghanstan katika kipindi cha siku 10 tu, wakachukua udhibiti wa miji kote nchini humo.

Wapiganaji wa Taliban waliuteka mji wao mkuu wa kwanza wa jimbo tarehe 6 Agosti-na kufikia tarehe 15 Agosti, walikuwa katika malango ya Kabul.

Mashambulio yao yaliyofananishwa kama radi yalisababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao, wengi wakiwasili katika mji mkuu Kabul, huku wengine wakikimbilia katika nchi jirani.

Na kulikuwa na ghasia katika mji wa Kabul, wakati Rais Ashraf Ghani alipotoroka nchi na maelfu ya raia wenzake wake kwa waume kutoroka pia.

Kuondoka vya vikosi vya Marekani

Wakipata ujasiri kutokana na kuondoka kwa vikosi vya Marekani na vingine vya kimataifa, mwezi Juni, Taliban walikuwa tareyio wamethibiti wa maeneo makubwa ya nchi.

Lakini baada ya tarehe 6 Agosti, kasi yao ya kusonga mbele iliongezeka huku wakiiteka miji zaidi.

Miji mikuu ya majimbo ilipinduliwa katika matukio ya haraka ya ukabidhianaji mamlaka.

Kufikia tarehe 8 Aprili, Taliban walikuwa wamechukua udhibiti wa Kunduz.

Herat, Lashkar Gah na Kandahar zilifuatia katika kipindi cha siku chache.

Kuanguka kwa vikosi vya Afghanstan

Licha ya miaka 20 ya usaidizi kutoka nje, mabilioni ya dola za msaada, mpango kabambe wa mafunzo na usaidizi wa ndege wa Marekani, vikosi vya Afghanstan viliangushwa pakubwa.

Hata jhivyo katika baadhi ya maeneo vilijikakamua na kupigana.

Katika jimbo la Lashkar Gah, vikosi vya Afghanstan vilirejeshwa nyuma na kuzuiliwa katika ngome zake, huku Taliban wakiwashambulia mara kwa mara

Mamia ya makomandoo walipelekwa kurejesha hali ya utulivu-lakini wakati Taliban walipofyatua mabomu mazito ya kutegwa ndani ya gari nje ya makao makuu ya polisi, tarehe 11 agosti, mapambano yalikuwa yameisha.

Katiak maeneo mengi, vikosi vya Afghanstan, ambavyo vilijipata vvikiishiwa silaha na vifaa vingine vya kijeshi vilitoroka.

Wanajeshi wenye silaha na ambao walipatiwa mafunzo na Marekani kuwalinda raia wa kawaida wa Afghanstan waliwaacha kwa kiasi kikubwa wajilinde wenyewe.

Na katika baadhi ya maeneo, maafisa walikubali kuwaruhusiu Taliban kuchukua udhibiti, ili kuzuia umwagaji damu zaidi.

Katika Ghazni, ripoti zinasema mkuu wa polisi na gavana wote waliruhusiwa kuondoka katika mji huo ili kuwaruhusu Wataliban kuutwaa.

Tarehe 14 Julai, Mazar-i-Sharif iliangukia mikononi mwa Taliban, kwa upinzani mdogo wa vikosi vya Aghanstan, ambao baadhii waliondoka mjini humo na kuelekea kwenye mpaka wa Uzbekistan katika eneo la Haraitan.

'Janga la kibinadamu'

Kufikia tarehe 15 Agosti , watu 17,600 waliokuwa wamekimbia mashambulio ya Taliban walikuwa wamewasili katika mji mkuu Kabul, huku maelfu wengine wakiwasili wakati wowote, kulingana na Ofisi ya Umoja wa mataifa ya uratibu wa masuala ya kibinadamu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakiwa na usaidizi mdogo sana kutoka kwa mamlaka za Afghanstan, wengi walikuwa wakilala nje katika bustani na maeneo mengine ya umma.

Baadhi walisema walikuwa wametoka katika miji iliyochukuliwa na Taliban ambako Taliban walikuwa wakiwauwa watu wa jinsia ya kiume katika family amnbao walikuwa wakifanyika kazi vikosi vya usalama, na kuweka tena sheria kali dhidi ya wanawake.

Shirika la mpango wa chakula duniani, lilisema kuwa mzozo huo ulikuwa na "ishara zote za janga la kibinadamu".

Vurugu mjini Kabul

Wakati rais Ghani alipoikimbia nchi, wahudumu wa ubalozi wa Marekani waliupandishwa katika helkopta ili kuwaondosha katika eneo limelindwa vikali.

Na maelfu ya watu walikuwa wakielekea katika uwanja wa ndege wa Kabul.

Wapihganaji wa Taliban mwanzoni walikuwa wametulia nje ya mji mkuu Kabul, wakati mazungumzo ya dharura yalipofanyika katika kasri ya rais.

Lakini waliiingia ndani ya mji ili kuchukua udhibiti wake kamili.

Hali ya baadaye isiyojulikana

Haikjulikani ni vipi hasa Taliban inalenga kuongoza - huenda utawala wake ukawa tofauti kote nchini.

Taarifa kutoka ndani ya eneo linaloshikiliwa na Raliban hadi sasa zinatoa picha mchanganyiko.

Katika Balkh, kilomita 20 (au maili 12 ) kutoka from Mazar-i-Sharif, BBC iliwapata wanawake na wasichana wakiruhusiwa kuwa katika maeneo ya umma bila kusindikizwa - lakini kulikuwa na ripoti za wanawake ambao waliuawa kwasababu ya jinsi walivyokuwa wamevaa.

Katika sehemu nyingine, mkiwemo maeneo ya wilaya ya vijij ya kaskazini katibu na mpaka wa Tajikistan, wanawake wamesema kuwa wanalazimishwa kujifunika kwa burka na hawawezi kwenda nje bila kusindikizwa.

Pia kuna ripoti za vijana wa kike wanaotolewa kwa Taliban kwa ajili ya ndoa ya kulazimishwa.

Ingawa wawakilishi wa Taliban waliopo Qatar wanasisitiza kuwa ni "uongo".