Vita vya Afghanistan: Fahamu mataifa yanayodaiwa kulifadhili kundi la Taliban

Wapiganaji wa kundi la Taliban

Kundi la wapiganaji wa Taliban limekuwa likikabiliana na vikosi vya serikali ya Afghanistan vinavyoungwa mkono na serikali ya Marekani kwa takriban miaka 20.

Serikali ya Afghnaistan imekuwa ikifadhiliwa na Marekani , lakini haijulikani ni wapi kundi la Taliban limekuwa likipata ufadhili wake katika vita hivyo.

Inaaminika kwamba kundi hili linatengeneza fedha nyingi kutoka ndani na nje ya nchi.

Halafu swali jingine ni hili, je wapiganaji hawa hupata silaha zao kutoka wapi?

Je Kundi Taliban hupata pesa ngapi?

Kundi la Taliban awali lilitawala Afghanistan kutoka mwaka 1996 hadi 2001, wakati ambapo uongozi wao ulikuwa chini ya sheria za kiislamu.

Tangu kuanguka kwa utawala huo, wamekuwa wakipigana kwa muda mrefu hadi walipoiteka tena nchi hiyo.

Mara kwa mara hutokea uvumi wa jinsi kundi hilo linavyojipatia fedha kwasababu lina usiri mkubwa wa jinsi linavyojifadhili.

Lakini mahojiano na wataalamu nje na ndani ya Afghanistan yaliofanywa na BBC yamebaini kwamba kundi hilo lina mtandao wa kuchangisha fedha katika hali ambayo haiwezi kufahamika.

Pia hukusanya kodi kufadhili operesheni zao.

Chanzo kikuu cha fedha zao ni uuzaji wa madawa kutoka taifa hilo.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mkulima wa Afghanistan akivuna tunda la mmea wa Opium

Jeshi la marekani limesema katika miaka ya hivi karibuni kwamba limeanzisha msururu wa mashambulizi dhidi ya hifadhi za madawa zinazoaminika kufadhiliwa na kundi la Taliban.

Lakini mapato ya kundi hilo hayatokani tu na biashara ya mmea wa Opium pekee.

Tangu mwaka 2011 , pato la kila mwaka la kundi hilo limekadiriwa kufikia £ 316m.

Lakini inaaminika kwamba pato hilo limeongezeka maradufu katika miaka ya hivi karibuni na kufikia $ 1.5bn.

Dawa ya kulevya Opium na kuwalizimishaa raia kulipa kodi

Afghanistan ndio taifa kubwa zaidi linalozalisha mti wa dawa kwa jina "Opium".

Mti unaotumiwa kutenegeneza dawa ya kulevya aina ya heroine

Uuzaji wa dawa hiyo unakadiriwa kuwa - kati ya $ 1.5- $ 3bn.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa serikali ya Aghanistan

Taliban hujipatia kodi yake kupitia viwango kadhaa vya ushuru unaowekewa raia.

Asilimia 10 ya kodi hiyo hutozwa wakulima wa mmea wa Opium.

Kodi hiyo hukusanywa katika maabara ya dawa za Opium.

Ushuru huo pia hutozwa watu wanaosafirisha dawa kwa njia haramu.

Fedha wanazokusanya Taliban kwa watu wanaosafirisha dawa kwa njia haramu zinakadiriwa kuwa kati ya $ 100m- $ 400m.

Madini

Afghanistan ni taifa tajiri lenye madini , mengi ambayo yalikuwa chini ya mikono ya watu binafsi wakati ambapo taifa hilo lilikuwa katika vita.

Mapato kutoka kwa madini ya Afghanistan yanakadiriwa kufikia $ 1bn kila mwaka. Madini mengi huchimbwa kwa njia ya haramu.

Maelezo ya picha,

Madini yanayouzwa mjini kabul

Kundi la wapiganaji wa Taliban husimamia migodi na kukusanya pesa kwa nguvu kutoka kwa wachimbaji madini haramu .

Mwaka 2014 , ripoti ya Umoja wa Mataifa ilisema kwamba Taliban ilijipatia $10m kila mwaka kutoka kwa migodi kati ya 25 hadi 30 kusini mwa mkoa wa Helmand.

Uwekezaji wa nje ya nchi

Maafisa wa Marekani na wenzao wa Afghanistan mara nyingi wameyashutumu mataifa 7 katika eneo hilo kwa kuwafadhili kifedha wapiganaji wa Taliban.

Mataifa hayo ni pamoja na Pakistan, Iran, Urusi lakini yamekana madai hayo.

Pia kuna ripoti za awali kwamba watu binafsi kutoka Pakistan na mataifa kadhaa ya Ghuba , kama vile Saudi Arabia , UAE na Qatar wanaaminika kujitolea kuunga mkono kifedha shughuli za kundi hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Huku ikiwa haijulikani haswa kiwango rasmi , wataalamu wanakadiria huenda ikafikia $ 500m, kila mwaka..

Je Kundi la Taliban linatoka wapi?

Licha ya uadui wa kihistoria uliopo kati ya Taliban na Urusi , Marekani inaamini kwamba serikali ya Moscow inalisaidia kundi hilo kijeshi.

Urusi hatahivyo imekana madai hayo. Waanzilishi wa kundi hilo walikuwa miongoni mwa wapiganaji wa kundi la Mujahideen waliokuwa wakipigana dhidi ya Muungano wa Usovieti 1980.

Baada ya Usovieti kuondoka Afghanistan, Urusi ilitoa usaidizi wa kifedha na kijeshi kwa kundi la Taliban.

Lakini wakati Marekani ilipoingia Afghanistan , kufuatia shambulio la Septemba 11, Taliban ilichukua fursa hiyo kushirikiana na Urusi.

Maafisa wakuu wa Marekani wanasema kwamba Moscow inasambaza silaha kwa Taliban , kulingana na wataalamu 2018.

Chanzo cha picha, Gen Nicholson

Katika mahojiano ya awali na BBC , kamanda wa vikosi vya Marekani jenerali John Nicholson, alisema madai kwamba Urusi ilikuwa inalifadhili kundi la Taliban Kijeshi yalikuwa ya kweli .

Wachunguzi wengi waliona hatua hiyo kuwa ishara ya vita baridi kati ya Marekani na Urusi.

Jenerali Nicholson ametangaza kwamba Urusi inasambaza silaha kwa Taliban kupitia mpaka wa Tajikistan.

‚'Kuna silaha zinazoingizwa nchini humu na viongozi wa Afghanistan na wanasema kwamba Urusi imekuwa ikiwapatia Taliban silaha hizo'' , alisema jenerali John Nicholson.

Urusi na Taliban zote zimekana matamshi ya jenerali huyo kwa BBC zikisema kwamba hakuna ushahidi.

Ubalozi wa Urusi uliopo mjini Kabul na wizara ya masuala ya kigeni ya Urusi zimekana madai hayo na kuyataja kwamba hayana msingi.