Vita vya Afghanistan:Mabilioni ya fedha na miaka zaidi ya 20 ya mafunzo yakosa kulisadia jeshi la Afghanistan

Wapiganaji wa kundi la Taliban

Chanzo cha picha, Getty Images

Agosti15, wanamgambo wa Taliban waliuteka mji mkuu wa Afghanistan, Kabul na kutangaza kuwa vita vimeisha.

Kasi ya radi iliyotumiwa na kundi hilo kuteka maeneo tofauti ya nchi hiyo huku Vikosi vya Afghanistan vya Ulinzi na Usalama wa Kitaifa wa kitaifa (ANDSF) vikirudi nyuma bila kupigana iliwashutua watu wengi.

Zaidi ya miaka 20 iliyopita, Marekani ilitumia zaidi ya dola bilioni 83 kuwapa mafunzo, kuwahami na kuunda jeshi la kitaifa la Afghanistan, polisi, jeshi la angani na vikosi maalum. Lakini kundi lililojihami kwa silaha nyepesi, lilifanikiwa kusambaratisha ANDSF kwa mtindo wa kuvutia.

Kasi hiyo isiyokuwa ya kiwaoda iliyotumiwa na Taliban kuteka maeneo ya Afghaistan pia ilishangaza ujasusi wa Marekani ambao ulikadiria itachukua kundi hilo miezi kadhaa kuchukua udhibiti wa nchi hiyo.

Kutokana na hatua hiyo Marekani na nchi kadhaa za magharibi zimelazimika kurejesha maelfu ya wanajeshi wao nchini Afghanistan ili kusaidia kuwaondoa raia wao na wafanyakazi wa kidiplomasia mjini Kabul.

Laiti wachambuzi na mashirika ya kijasusi ya magharibi hayakuwa na uelewa wa hali halisi nchini humo, pengine wangelipatikana ghafla katikati ya matukio ya siku chache zilizopita

Masuala kadhaa yalichangia kuanguka kwa utawala wa Afghanistan na vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo ANDSF.

Chanzo cha picha, AFP

Kwanza ni kukithiri kwa ufisadi katika wizara ya Ulinzi na mambo ya ndani ya Afghanistan ambako fedha, silaha na misaada ya chakula iliibiwa kabla ya kuwafikia wanajeshi waliyoko nyanjani.

Silaha na vifaa vingine viliuzwa kimagendo na hatimaye kufikia mikononi mwa Taliban.

Kando na hilo, baadhi ya makamanda walifuja fedha kwa kuwasilisha ombi la mishahara ya "askari hewa" - yaani wanajeshi ambao hawakuwa wamejiandikisha kwa jeshi.

Hayo yakifanyika wafanyakazi wa ANDSF waliendelea kuhudumu bila kulipwa mishahara na kuzuiwa ruhusa ya kuona familia zao. Haishangazi, ANDSF ilikuwa na moja ya kiwango cha juu cha kutengwa na majeruhi ulimwenguni. Kulingana na moja ya makadirio kiwango cha uwandani wa ANDSF kwa mwezi kilikuwa 5,000 wakati kiwango cha kuajiri kilikuwa 300 hadi 500.

Pili, ubadhirifu na ufisadi ulidhoofisha ari ya utendaji ndani ya jeshi. Uadilifu wa uongozi wa juu ni muhimu katika maswala ya jeshi kushinda heshima na uaminifu wa wanajeshi.

Kwa wanajeshi ambao hawajalipwa, mtindo wa maisha wa kifahari wa makamanda wao mara nyingi ulikuwa unawaumiza. Kwa hivyo, badala ya kupigana na kufa, waliamua kuokoa maisha yao kwa kujisalimisha kwa Taliban chini ya ofa yake ya msamaha.

Chanzo cha picha, Getty Images

Tatu, Hakukuwa na mshikamano wa kiitikadi ndani ya jeshi au hali ya jukumu la kitaifa na mali. Kwa kweli, kulikuwa na kutokuaminiana katika uongozi wa kisiasa wa nchi hiyo.

Mazingira haya ya kutoaminiana na mashaka yalizidi kudhoofisha azimio la wanajeshi wa Afghanistan kukabiliana na Taliban ambao wapiganaji wao walikuwa na mshikamano wa kiitikadi, na hamu ya kuunda taifa la Kiislamu na kuwafukuza wanajeshi wa kigeni waliowaona kama wavamizi.

Nne, Muingilio wa kisiasa wa mara kwa mara na kubadilishwa kwa wakuu wa ngazi ya juu kama mawaziri wa mambo ya ndani na ulinzi, magavana na wakuu wa polisi pia kuliathiri utendaji wa ANDSF.

Jeshi linahitaji umoja wa amri na mwendelezo wa uongozi ili kufanya kazi vizuri na kupigana vyema kwenye uwanja wa vita. Mkuu wa jeshi ni kiungo muhimu na mvuto mkubwa kwa vikosi vyake na ikiwa atabadilishwa kila wakati, bila shaka jeshi litaathirika.

Rais Ghani mara kwa mara alibadilisha viongozi wake wa jeshi licha ya Marekani kuanza kuondoa vikosi vyake na mashambulizi ya Taliban kote Afghanistan.

Kwa mfano, Ghani alichukua nafasi ya mkuu wa jeshi la Afghanistan Luteni Jenerali Wali Mohammad Ahmadzai, ambaye aliteuliwa mnamo Juni, na kamanda maalum wa operesheni ya Jeshi la Kitaifa la Afghanistan, na kumpatia Meja Jenerali Haibatullah Alizai.

Pia alifanya mageuzi mara mbili katika wizara ya mambo ya ndani na kuleta mabadiliko katika wizara ya ulinzi na kwa kuwageuza makamanda sita muhimu katika miezi ya hivi karibuni.

Tano, mkakati mzuri wa kijeshi wa Taliban wa kudhibiti mipaka muhimu, barabara kuu na kuzingira miji mikubwa ililemaza uwezo wa Kabul kutuma msaada na vifaa. Vikosi vingi vya jeshi vilitenganishwa na nchi nzima kwa hivyo, walilazimika kukimbilia katika nchi jirani za mipakani au kusalimu amri.

Mwishowe, licha ya kupata mafunzo ya miaka kadhaa na vifaa vyenye thamani ya mabilioni ya dola, ANDSF haijawahi kukuza uwezo wa kujisimamia yenyewe.

Ukweli ni kwamba, ilikuwa inategeme wanajeshi wa Marekani na NATO kulinda maeneo ya mijini.

Vikosi hivyo vilipoanza kuondoka, hakukua na chochote ambacho kingeliwazuia wapiganaji wa Taliban. Udhaifu na uwezo wa jeshi la taifa ulidhibitishwa na kuwepo kwa wanajeshi hao wa kigeni.

Ijapokuwa hofu ya kuanguka kwa ANDSF ilionekana wazi, utawala wa Afghanistan ulijitahidi kubuni kikosi kipya kilichoundwa kutokana na wanamgambo wanaounga mkono serikali.

Wababe watatu mashuhuri wa kivita - Atta Muhammad Noor of Jamiat-e-Islami, Abdul Rashid Dostum of Hezb-e-Junbish na Haji Muhammad Muhaqiq of Hezbe-e Wahdat Islami Mardom-e Afghanistan -walikutana kuandaa mikakati ya kukabiliana na Taliban na kuratibu mipango yao kwa ushirikiano na ANDSF.

Hata hivyo, kutekwa kwa Mazar-i-Sharif na wanamgambo wa Taliban kuliwalazimisha kukimbia nchi. Kuanguka kwa ANDSF hata kabla ya Marekani kukamilisha shughuli ya kuondoa vikosi vyake nchini humu na kujivunia mafanikio ya kile kinachoitwa "vita dhidi ya ugaidi" mambo yalibadilika kumesambaratisha juhudi zilizofikiwa miaka 20 iliyopita.

Maelfu ya wapiganaji walioachiliwa na Taliban kutoka kambi ya kijeshi ya Bagram, pamoja na wale wa al-Qaeda na makundi mengine, sasa yatakuwa changamoto kubwa kwa usalama wa Afghanistan.