Hawa ni viumbe 10 wa ajabu wanaopatikana baharini

a

Chanzo cha picha, Asher Flatt/NESP Marine Biodiversity Hub/CSIRO)

Viumbe wa ajabu wanapatikana kila mahali, wapo wanaofahamika na wasiofahamika. Wapo wanaoishi angani, ardhini napo wanaoishi majini ambao ndio hasa tunawatazama katika Makala haya.

Kwa mujibu wa wanasayansi kuna mamilioni ya viumbe wa majini wanaoishi na kupatikana kwenye vyanzo mbali mbali vya maji kama mito, maziwa na bahari. Lakini wengi wanaofahamika ni samaki wanailiwa na wasioliwa lakini ukweli ni kwamba kuna viumbe wengi wa ajabu kuwahi kushuhudiwa duniani wanaoshi baharini kama walivyobainika mwaka 2017 na wanasayansi mbalimbali. Miongoni mwao ni hawa.

Ratfish

Chanzo cha picha, Getty Images

Hii ni aina mpya ya Papa ambaye amegunduliwa mwaka huu Januari, huko Afrika Kusini na kuweka rekodi mpya. Ana urefu wa karibu futi 3 kama mita moja hivi, akiwa anashika nafasi ya pili kwa ukubwa kwa aina ya Papa walioogundulika . Hiyo ni kwa mujibu wa watafiti wa Pacific Shark Research Center huko California, Marekani.

Aina hii ya Papa wa ajabu ni ya 50 kugundulika duniani na ni wa tatu kwenye kundi la Hydrolagus, kwa maana ya "panya wa majini. Muonekano wake unatisha na ndio hasa sababu ya kupewa jina la Ratfish ama Ghost Shark.

Watafiti wanamuona papa huyu kama sio papa kwa sababu ya muonekano wake unaotisha na wa ajabu lakini akiwa na sifa za kufanana kiasi na mapezi makubwa zaidi yanayomtofautisha papa wa aina hii na papa wa kawaida wenye mkia wa kipekee.

Cannibal corpse

Chanzo cha picha, James Ormiston

Kiumbe kingine cha ajabu kilichogunduika mwezi Februari 2017 karibu na mji wa Moosonee kwenye uwanda wa Hudson Bay huko Ontario, Canada. Anafahamika pia kwa jina la Bobbit worm kwa maana ya Minyoo ya majini ya Bobbit.

Ni kiumbe kikongwe zaidi kilichowahi kuishi miaka 400 million iliyopita , na kufanya kuwa minyoo mikongwe zaidi kuwahi kuishi duniani. Kutokana na maumbile yake na taya zake, Bobit ana uwezo wa kujirefusha na kufikia urefu wa futi 3. Kwa sababu ya ukubwa wake, watafiti wametoa jina la Websteroprion armstrongi.

"Cosmic" jellyfish

Chanzo cha picha, NOAA

Samaki huyu anapatika kwenye maji yenye kina kirefu zaidi , anapenda kuishi kwenye kina cha kuanzia angalau futi 9,800 kama urefu wa kilometa 3 chini ya maji. Amegundulika kwenye kina cha bahari ya Pasific karibu na Samoa, akitajwa kama aina mpya ya jellyfish.

Ni ngumu kumuelezea alivyo, lakini umbuile lake lilionekana kwa mbali kupitia National Oceanic and Atmospheric Administration (NOAA), waliokuwa wanaendesha shughuli za kuzamia maji.

Walitumia kifaa cha kuonea vitu vilivyo mbali (microscope) na kusaidia kumgundua na kugundua wanapopatikana. "Tulivyokuwa tunaendelea kuangalia , tukaanza kupata picha ya namna maisha yalivyo huko chini ya maji -pengine ni makazi makubwa zaidi ya viumbe wa aina hii," alisema Michael Ford, mtaalam kutoka NOAA.

Shipworm

Chanzo cha picha, Marvin Altamia

Anafahamika kitaalamu kama Slimy mollusks au Shipworms, wanaotajwa kula mbao na wanaweza kuuchangamkia na kuumaliza mtumbwi ama boti ya mbao kwa muda mfupi..

Ni minyoo mikubwa yenye mkia wa ajabu ambao huwekwa kwenye kundi la Kuphus polythalamia, ingawa, kwa muda mrefu wa miaka na miaka haikuwahi kuonekana mpaka mwezi Aprili mwaka huu.

Watafiti walikusanya minyoo hii mitano kutoka kwenye mkondo mmoja huko Philippines kwa ajili ya kuifanyia utafiti. Tofauti na minyoo ya kawaida, minyoo hii inayokula mbao ina urefu wa kati ya futi 3 mpaka 5 ni kama mita moja mpaka mita 1 na nusu. Inaishi katika matope, na hujizungusha katika magamba magumu yanayoonekana kama mkonga wa tembo.

Lizard fish

Chanzo cha picha, NESP Marine Biodiversity Hub

Wanasayansi walikuwa wamepanda boti kutafuta samaki mashariki mwa pwani ya Australia, walipokutana kwa bahati mbaya tena bila kutegemea na kiumbe huyu anayejulikana kama Bathysaurus ferox, mweye muonekano wa sura kama mjusi na anayetajwa kama kiumbe hatari kinachoishi kwenye kina kirefu cha maji:

Anaishi kwenye kina cha bahari chenye urefu wa futi 3,300 mpaka 8,200 kama kilometa 1 mpaka kilometa 2.5 kutoka kwenye usawa wa bahari.

Akiwa anaogelea, matezi yake yanadaka vyakula. "Kama atafanikiwa kukudaka kwenye matezi yake, hauna la kufanya: Namna utakavyokuwa unapambana ujiondoe, ndo unavyozidi kutitita kwenye mdomo wake," Asher Flatt, aliandika mmoja wa wanasayansi hao waliokuwa kwenye boti.

Loch Ness

Chanzo cha picha, James Campbell

Ukifikiria kuhusu kiumbe huyu wa ajabu Loch Ness, pengine akilini mwako picha itakayokujia haraka ni ya plesiosaur — au madinosa yenye shingo ndefu na mabawa manne, au kiumbe mwenye ummbo la mamba.

Mapema Agosti 23 mwaka 2017, watafiti waliwasilisha utafiti wao kuhusu kiumbe mwenye umri wa miaka milioni 76 alioyeonekana huko Alberta, Canada.

Kiumbe huyu alikuwa na 'ukubwa wa kama gari'— akiwa na urefu wa futi kati ya 13 mpaka 16 sawa na mita kati ya 4 mpaka 5. Alikuwa hai kabisa kwa mujibu wa watafiti kutoka chuo kikuu cha Calgary.

Ingawa kwa kimo hicho ana onekana mkubwa, lakini watafiti wanasema ukumbwa wake unaweza kufikia mpaka futi 50 ama mita 15, ukubwa wa kama basi la kisasa la abiria.

Diamond Squid

Chanzo cha picha, Jay Wink/Abc Scuba Diving Port Douglas

Kiumbe hiki kimeonekana katika bahari karibu na Australia, kiasi cha kushangaza dunia kilipoonekana mwezi September mwaka 2017.

Muonekano wake, ni kama mnyoo si mnyoo, au kiumbe ambacho ni kama kipya kabisa kuwahi kuonekana duiani. Rebecca Helm, mtafiti kutoka Woods Hole Oceanographic Institution huko Massachusetts, Marekani, alitegua kitendawili hicho:

"Kiumbe hiki kiko kundi la Thysanoteuthis rhombus sakifahamika kwa jina linguine kama 'diamond squid', lakini ni ngumu kusema ni nani hasa," Helm aliiambia Live Science.

Diamond squid anaweza kukua kwa urefu wa futi mpaka 3, uzito wa kilo mpaka 30. Kiumbe hiko kinaweza kutaga mayai mpaka 24,100 mpaka 43,800 kwa wakati mmoja katika mudo wa kama bomba unaoweza kukua mpaka urefu wa futi 6 kama mita 1.8, kwa mujibu wa Helm.

Kleptopredator

Chanzo cha picha, Gabriella Luongo

Kiumbe kingine cha ajabu kinachopatikana majini anayefahamika kama Cratena peregrina na wanaopenda kula viuvimbe vinavyojitokeza ama vilivyopo katika viumbe vingine, igawa wanasayansi wengine wanasema kiube hiki hupenda kula viuvimbe baada ya kumaliza kula mlo wake mkuu hasa wa nyakati za jioni.

Deep-ocean shark

Chanzo cha picha, Kelvin Aitken/VWPics/AP

Wavuvi wanaovua ahari ya kina kirefu huko Ureno kwa bahati mbaya walimvua kiumbe huyu mwezi Novemba 2017.

Wanasayansi hao walikutana na kiumbe hiki cha ajabu kinachojuikana kama Chlamydoselachus anguineus — mwenye meno makali. Kwa mujibu wa watafiti kiumbe hiki kimekuwa na mabadiliko katika kipindi cha miaka milioni 80 kiasi cha kuelezewa na watafiti kama "living fossil."

Anatajwa kuwa na meno 300, ambayo ni makali na yanatisha akiwa na urefu unaoweza kufikia futi 5. Kiumbe hiki ni ngumu sana kuonekana na watu kwa sababu kinapenda kuishi na kuogelea kwenye kina kirefu kama futi 4,600 kama mita 1,400 au kilometa 1.4 kutoka usawa wa bahari

Bone-filled fish

Chanzo cha picha, Getty Images

Bonny fish mzito zaidi kuwahi kuvuliwa duniani ni yule aliyepatikana kwenye fukwe za Japan mwaka 1996. Alikuwa na kilo 2,300. Kwa iongo kadhaa sasa, wanasayansi wakisema aina hiyo ya samaki ama kiumbe ni kutoka kundi la Mola mola.

Lakini kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa baadae mwaka huo huo wa 2017, mwezi Disemba, na jarida la Ichthyological Research, kiumbe hiko kilichovuliwa ama kupatikana Japan kinafahamika kama Mola alexandrini.

Miili yao ni mikubwa na ya umbo la duara kiasi na wanaweza kukua mpaka urefu wa futi 10. Kwa sababu ya urefu na uziito wao huo, imekuwa ngumu kiumbe hiki kusafirishwa