Je unafahamu viumbe wanaoweza kubadilika maumbile na kuwa viumbe wenye muonekano tofauti na wao wa asili?

Bassettia pallida

Chanzo cha picha, Andrew Forbes/Universidad de Iowa

Maelezo ya picha,

Bassettia pallida ni vimelea wanaosababisha maambukizi kwenye miti ya aina ya elm kulingana na ugunduzi wa hivi karibuni

Mazombi ya kutisha tunayoyafahamu kwenye filamu za kufikirika huonekana ya kutisha , yakila nyama za watu na huwa yanaoneshwa kama viumbe wanaoishi baada ya kifo.

Na ingawa hadithi hizo hazijawahi kuwa za kweli, dunia huwa imejaa visa vya aina hiyo vinavyofanana na yanayoshuhudiwa katika filamu hizo.

Kuna jambo linaloshangaza kuhusu wazo kwamba tabia ya wanyama inaweza kubadilika kwa kiasi kikubwa kutokana na maambukizi au vimelea, lakini hili limebainika kuwa ni jambo ambalo limekuwepo kwa kwa muda mrefu na la asili.

Ukweli ni kwamba, masalia ya viumbe wa kale hutoa ushahidi wa uwepo wa mazombi ya mchwa - kwa kuangalia alama zilizopo kwenye miili yao iliyopatwa na maambukizi- miaka milioni 48 iliyopita.

mabadiliko ya maumbile yaliyosababisha mazombi ya mchwa

Utafiti uliofanyika nchini Thailand na jopo la kimataifa ulioongozwa na David Hughes wa Chuo cha jimbo la Pennsylvania ulifichua jinsi kuvu la Ophiocordyceps unilateralis lilivyojitengeneza na kubadilisha umbile la vichwa vya mchwa wa maeneo ya joto ( Camponotus Leonardi ).

Kuvu hili linalofahamika kama Ophiocordyceps unilateralis liliwezesha vimelea wa eneo hilo kuangamia chini ya jani.

Haijafahamika wazi ni kwa jinsi gani kuvu lina athari hizi za kushangaza na za kipekee kwenye viumbe wagumu zaidi kuliko kuvu lenyewe.

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha,

PICHA: Mchwa wa maeneo ya tropiki mwenye aliyeambukizwa kuvu lenye uwezo wa kusababisha maambukizi

Lakini David Hughes, Harry Evans, na wenzake wamegundua kwamba viumbe tofauti wa Ophiocordyceps unilateralis wamebadilika ili kuweza kuendana na mizunguko tofauti ya maisha ya spishi ambao wanawachukua kama wathiriwa wao

Ni " mfano wa kuvutia wa mabadiliko ya kimaumbile , " anasema Evans.

Katika makala ya mwaka 2016 , Evans na waandishi wengine wa utafiti walielezea kwamba kuvu lina uwezekano mkubwa wa kutumia vimeng'enyo kadhaa ambavyo hubadili utendaji katika miili ya michwa.

Ingawa haijathibitishwa, inaweza pia kunaweza kuwa na ubadilishwaji wa moja kwa moja wa mfumo wa neva wa mchwa, na udhibiti wa mfumo wa neva "jumbe za kikemikali " kama vile dopamine, ambayo inaweza kubadilisha tabia ya mchwa.

Kubadilishwa kwa umbile la nyigu

Wakati maisha ya viumbe wawili yanahuisiana moja kwa moja -kama vimelea m na kuvu - ni faida kwa viumbe wote wawili.

Katika ulimwengu wa mdudu kuna mifano mingi , kama vile nyigu, ambao migu yake yake inaweza kutandazwa juu ya wadudu kama viwavi

Wakati mayai yanapoanguliwa, lava za nyigu huingia kwenye majimaji ya mwili ya viwavi kabla ya kutunga hariri kando pembeni.

Chanzo cha picha, Andrew Forbes/Universidad de Iowa

Maelezo ya picha,

Nyigu anavyotengenezwa kama mdudu ni sawa na kuandika filamu ya kutisha

Ingawa kiwavi huharibiwa katika mchakato huo, bado huendelea kuwa hai na kuwa kama aina fulani ya zombi ambalo huwa na nguvu na kuangusha kila mende anayekaribia hariri na huweza kushambulia hariri inayolinda mayai.

Uvumbuzi huu ulifanyika baada ya mtafiti mwenza wa Weinersmith -Scott Egan, kuvumbua nyigu aiye wa kawaida aliyekuwa aliruka alipokuwa katika matembezi na familia yake wakati wa likizo. Nyigu huyu alitengenezwa na spishi wanaoitwa Basettia pallida .

Kwa kawaida B. pallida hutoka katika yai na hutengeneza shimo katika kuvimba mwili wake kabla ya kupaa.

Chanzo cha picha, Egan Lab/Rice University

Maelezo ya picha,

PICHA:Nyigu aina ya 'Bassettia pallida' hufa katika mashimo waliyoyatengeneza

"Hatujui utaratibu unaotumiwa, lakini hupata nyigu wa kwanza ambaye alikuwa pale kubuni shimo la kuchungulia ," Weinersmith anaelezea.

"Ni mdogo kuliko umbo la kawaida la nyigu na badala ya kutoka nje, miguu yake hukwama na hufa akiwa amekwama kwenye shimo lile ."

Nyigu huyu aina ya Euderus set hukwama kwenye shimo kadri anavyokuwa

"Anapomaliza kukua, huonekana vichwa vichwa vyao vimeungana na kuvu " anasema mwanasayansi.

Hapo ndipo vimelea huzaa vimelea.

Nyigu wa kwanza B. pallida , mwenyewe ni kimelea wa tatu, amekuwa aina ya zombie wa kujitola mhanga ... na chakula chenye vitutubisho kwa vimelea wake mwenyewe, (Euderus set ).

Mazombi wa ngono

Lama Zombi ni kiumbe ambaye tabia yake imebadilishwa haraka kwa ajili ya faida ya vimelea wake, basi mfano mwingine wa ajabu unaweza kupatina miongoni mwa vyura wa mitini wa Japan wa Korea Kusini .

Mwezi Machi 2016, Bruce Waldman kutoka Chuo kikuu cha taifa cha Seoul na mwanafunzi wake Deuknam walichapisha ushahidi wa tabia zisizo za kawaida ujanja zilizosabishwa na kuvu wanaosababisha magonjwa au , Batrachochytrium dendrobatidis.

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha,

Vyura wa mtini wa Japan hubadili sauti wanaoyoitoa wanapoambukizwa na vimelea wa magonjwa 'Batrachochytrium dendrobatidis'.

Kuvu hawa wanafahamika vyema kama tisho kwa spishi wengi wa vyura, lakini vyura wa mtini wa Japan wanaopatikana barani Asia hawaonekani kufa mara moja wakati wanapoambukizwa na vimelea hawa.

Wakati Waldman na An waliposikia sauti za vyura 42 wa mtini , walibaini kuwa tisa kati yao walikuwa wameambukizwa na Batrachochytrium dendrobatidis , sauti zao zilikuwa za haraka na za muda mrefu, na kuzifanya kuwa za kuvutia kwa wenza wao.

Matt Fisher anasema kuwa jamii hawa wa Amphibia huenda walibadilika kuwa "mazombi wa ngono," ambao mahusiano yao ya mara kwa mara na wapenzi wao huenda yaliongeza uwezekano wa kuvu kusambaa mbali.

"Sio utafiti uliothibitishwa, lakini data zake ni imara ," anasema.

Mabadiliko ya maumbile ya mimea inayoifanya kuwa Zombi

Huenda mifano zaidi inayojitokeza ya maisha halisi ya Zombi katika wanyama wa mwituni haiku katika wanyama, bali katika mimea ambayo hubadilika na kuwa katika maumbile mapya ya mimea yenyewe.

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha,

Janipanzi linaweza kusambaza bakteria kutoka mmeaplant in Swahili

Saskia Hogenhout kutoka kituo cha John Innes, na wenzake waligundua utaratibu ambao kikundi cha baktetia , phytoplasma, hubadili mme kuwa katika hali ya kushindwa kujilinda dhidi ya kuwa mazombi . Walichapisha utafiti wao mnamo mwaka 2014.

Bakteria husika anahitaji kusambazwa na wadudu wanaokula mmea, kwa mfano panzijani.

Lakini ili kuvutia bakteria hawa, mmea ulioambukizwa lazima uwe umeinama kulingana na matakwa ya bakteria.

Protini inayoingia huchukua nafasi ya mimea yenyewe wakati mmea unpoanza kubadilika kimaumbile.

Maua huanza kubadilika rangi na kuwa kijani, kwa maana nyingine hugeuka na kuwa majani .

Maambukizi huyafanya majani kuwa ya kuvutia zaidi kwa wadudu, ambao hupata bakteria na kuwapeleka kwenye mimea mipya.

Chanzo cha picha, SB Johnny/CC 3.0

Maelezo ya picha,

Maua ya kijani yaliyosababishwa na 'Aster Yellows Phytoplasma' katika solidago.

Mimea ya Zombi ni mifano ya kuvutiakwasababu mmea wenyewe haufi kutokana na maambukizi.

Badala yake inakuwa muhimu katika kuendelea maambukizi baina ya mimea.

Kama Mwanabaiolojia Jon Dinman kutoka Chuo Kikuu cha Maryland alivyoelezea baadhi ya mtindo wa maambukizi ya 'zombi' yaliyofanikiwa ya 'mazombi'' some huifanya mimea kuendelea kuishi.

Kwa ujuma, ugonjwa una uwezekano mkubwa wa kusambazwa kati ya viumbe wakati uwezo wake wa kujidhuru unapoweza kudhibitiwa

Hili ndilo jambo halisi linalotokea katika mimea ya zombi.

Kwa bahati nzuri, binadamu hawatishiwi na vimelea hawa wa magonjwa.

Wadudu na viumbe wengi pia hawana tisho hilo.

Katika misitu katika maeneo mbali mbali ya dunia, tayari zombie wako pale, akili na miili yao vilibadilishwa kutokana na vimelea.