Fahamu nchi 10 duniani zinazotumia utajiri wao mwingi kununua silaha?

Caza F35

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ndege ya kivita aina ya F35 ndio silaha ya gharama ya juu zaidi katika historia ya Marekani.

Jumla ya matumizi ya kijeshi ulimwenguni yalifikia $ trilioni 1.7 mnamo 2017. Na Marekani peke yake ilitumia dola bilioni 610 mnamo mwaka 2017.

Uchumi unaoongoza ulimwenguni pia ndio nchi inayotumia pesa nyingi zaidi kwenye Ulinzi, lakini hata sio yenye "mzigo mkubwa kijeshi" huku wataalam wakitaja uzito wa matumizi ya Ulinzi na kuzingatia utajiri unaozalishwa na kila nchi, unaopimwa kulingana na Pato la Taifa (GDP).

Mnamo mwaka wa 2017, matumizi ya jeshi la Marekani yaliwakilisha asilimia 3.1 ya Pato la Taifa - GDP, ambayo ni sawa na zaidi ya robo ya asilimia iliyotumiwa na nchi hiyo ambayo matumizi yake ni ya juu zaidi, kulingana na makadirio ya Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (Sipri).

Kwa kweli, na matokeo haya, Washington haiingii hata kati ya majimbo 20 ambayo hutoa utajiri wao mwingi kwa sekta ya Ulinzi.

Fahamu mataifa 10 yanayoongoza katika orodha hiyo.

10.- Bahrain

Chanzo cha picha, Getty Images

Bahrain ni fungu la visiwa linalotawaliwa na utawala wa kifalme wa Kisuni lakini wengi wa wakaazi wake milioni 1.4 ni Waislamu wa Kishia, ambako kumekuwa sababu ya mivutano mingi ya ndani.

Mnamo mwaka wa 2011, wakati wa ghasia katika kile kinachoitwa vuguvugu la Uarabuni, vikosi kutoka Baraza la Ushirikiano la Ghuba vilipelekwa nchini humo kusaidia kudhibiti maandamano.

Mnamo mwaka 2017, ilitenga $ milioni 1,396 kwa matumizi yake ya ulinzi, ambayo ni sawa na karibu $ 936 kwa kila mtu na asilimia 4.1 ya Pato la Taifa, kulingana na makadirio ya (Sipri).

9.- Urusi

Urusi ilisajili kupungua kwa mara ya kwanza kwa matumizi yake ya kijeshi kwa asilimia 20 tangu 1998, karibu dola za Marekani milioni 66,335, sawa na asilimia 4.3 ya Pato la Taifa (GDP).

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Urusi imeweka kipaumbele katika kuhakikisha majeshi yake yanakuwa ya kisasa.

Kulingana na Siemon Wezeman, mpelelezi mkuu wa Sipri, kupungua huku ni matokeo ya matatizo ya kiuchumi ambayo yamekuwa yakikumba nchi hiyo tangu mwaka 2014, kwani kwa Moscow kufanya Jeshi lake kuwa la kisasa kumeendelea kupewa kipaumbele.

8.- Lebanon

Kati ya majimbo 10 yaliyo na "mzigo mkubwa wa kijeshi" duniani, sita ni ya Mashariki ya Kati na Lebanoni ni moja wapo.

Nchi hiyo ilikumbana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu kati ya mwaka 1975 na mwaka 1990 na tangu wakati huo, maisha yake ya kisiasa yamekuwa na mgawanyiko mkubwa wa ndani.

Sera yake ya ndani na nje imeshawishiwa na nchi jirani ya Syria, pamoja na kundi la Kiislam la Hezbollah, ambalo mnamo mwaka 2006 lilipigana vita na Israeli.

Matumizi yake ya ulinzi mnamo mwaka 2017 yalifikia dola za Marekani milioni 2,441, sawa na asilimia 4.5 ya Pato la Taifa (GDP).

7.- Israeli

Tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1948, Israeli imezungukwa na nchi zenye uhasama nayo.

Hali hii ilitulizwa kidogo kutokana na makubaliano ya amani yaliyosainiwa na Misri mwaka (1979) na Jordan (1994).

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kwasababu imezoea kuwa imezingirwa na maadui, Israeli imewekeza pakubwa katika jeshi.

Hata hivyo, inaendelea kuwa na wapinzani kwenye mipaka yake kama serikali ya Syria na wanamgambo wa Hezbollah wa Lebanon, washirika wa Iran, mmoja wa wapinzani wenye nguvu zaidi wa serikali ya Kiebrania.

Kulingana na Sipri, matumizi ya jeshi la Israeli mnamo mwaka 2017 yalikuwa dola za Marekani milioni 16,489 (asilimia 4.7 ya Pato la Taifa - GDP).

6.- Jordan

Jordan ilipata uhuru wake mnamo mwaka 1946 na tangu wakati huo imekuwa ikikabiliwa na mivutano mingi inayotokana na mazingira ya kutatanisha.

Mnamo mwaka wa 1967, wakati wa Vita vya Siku Sita dhidi ya Israeli, ilipoteza udhibiti wa Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki, maeneo ambayo ilikuwa imechukua tangu vita vya kwanza vya Waarabu na Israeli mnamo 1948.

Mnamo mwaka 1984, alisaini makubaliano ya amani na Israeli, ambayo haiiwachilii kutokana na shida zingine za usalama ambazo zinatatiza eneo hilo, kama tatizo la lilijitokeza kwenye Jimbo linalojiita la Kiislamu.

Mnamo mwaka 2017, ilijitolea $ milioni 1,939 kwa eneo la ulinzi (asilimia 4.8 ya Pato la Taifa).

5.- Algeria

Algeria imekumbana na visa vya vurugu kali katika historia yake kama taifa huru lililoanza mwaka 1962. Mengi ya haya yametokana na mvutano kati ya sekta za kidini na za kidunia za jamii yake.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Algeria imekumbwa na mashambulizi kadhaa ambayo yametekelezwa na Al Qaeda ya Maghreb ya Kiislamu.

Kati ya mwaka 1992 na 1998, nchi hiyo imekumbana na mzozo mkali wa ndani ambao ulisababisha vifo zaidi ya 100,000 baada ya kufutwa kwa uchaguzi ambao ilionekana kuwa chama cha Islamic Salvation Front kingeibuka na ushindi.

Tangu wakati huo, nchi hiyo imeendelea kuathirika na waasi wa Kiislam wa kiwango cha chini, lakini pia imekabiliwa na mashambulizi kutoka kwa vikundi vya kitaifa kama vile Al Qaeda ya Maghreb ya Kiislamu.

Katika mwaka 2017, ilirekodi matumizi ya Ulinzi yaliyokadiriwa na Sipri kuwa dola za Marekani milioni 10,073, sawa na asilimia 5.7 ya Pato la Taifa.

4.- Kuwait

Ikiwa na eneo la kilomita za mraba 17,818 tu na chini ya wakaazi milioni tatu, Kuwait ni kifalme ndogo iliyozungukwa na majirani wenye nguvu: Saudi Arabia, Iran na Iraq.

Nchi hiyo ina vituo kadhaa vya jeshi la Marekani ambapo sehemu ya vikosi vya muungano wa kimataifa vinavyopambana na kile kinachoitwa Islamic State .

Mnamo mwaka 2017, ilikuwa na matumizi ya kijeshi ya dola za Kimarekani 6,831, sawa na asilimia 5.8 ya Pato la Taifa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Maonyesho ya silaha za kimataifa Kuwait.

3.- Congo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni nchi ya Kiafrika inayotenga sehemu kubwa ya utajiri wake kwa sekta ya ulinzi ikiongeza dola za Kimarekani milioni 484 kwa mwaka 2017, kulingana na makadirio ya SIPRI.

Nchi hiyo imepitia mizozo mingi tu ya ndani kwa ndani na inaongozwa na Denis Sassou-Nguesso, mwanajeshi wa zamani ambaye alitawala nchi kati ya 1979 na 1992 na ambaye alirudi mamlakani mnamo mwaka 1997, ambapo ameendelea kuhudumu hadi sasa.

2.- Saudi Arabia

Tangu mwaka 2015, serikali ya Saudi Arabia imeongoza kundi la nchi zinazopigana Yemen dhidi ya majeshi ya Houthi ambayo yanakabiliwa na Rais Abdrabbuh Mansour Hadi na yanaungwa mkono na Iran.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Majeshi ya Saudi Arabia yaliongoza operesheni ya muungano wa kimataifa katika mapigano ya Yemen.

Hali hiyo ni moja tu kati ya matukio kadhaa ambayo Riyadh na Tehran wanapigania kuwa na udhibiti wa eneo.

Mfalme wa Saudia pia hushiriki katika muungano wa umoja wa kimataifa dhidi ya kundi linalojiita Islamic State.

Kulingana na Sipri, mwaka 2017 nchi hii ilitenga dola milioni 69,413 za Marekani kwa matumizi ya kijeshi (asilimia 10 ya Pato Ghafi la ndani la Taifa).

1.- Omán

Nchi hiyo iliyopo kimkakati kuvuka Mlango bahari wa Hormuz, moja ya vivuko muhimu vya haidrokaboni, na majirani kama Iran, Saudi Arabia na Yemen, Oman imeongeza kwa kasi matumizi yake ya kijeshi katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Kwanza, kiukweli, ilikuwa nchi ulimwenguni ambayo ilitumia pesa nyingi zaidi katika ulinzi wake.

Mnamo mwaka 2017, matumizi yake ya kijeshi yalikuwa dola za Marekani milioni 8,686, ambayo ni sawa na asilimia 12 ya Pato la Taifa.