Shambulio la uwanja wa ndege wa Kabul: Je! Tunajua nini?

Medical and hospital staff bring an injured man on a stretcher for treatment

Chanzo cha picha, Getty Images

Milipuko miwili ikubwa ya mabomu yenye nguvu imegonga mwambao wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai mjini , wakati raia wakiendelea kutafuta njia ya kutoroka Afghanistan inayodhibitiwa na Taliban.

Karibu watu 60 wameuawa na wengine 140 kujeruhiwa, afisa wa afya wa ngazi ya juu mjini Kabul ameiambia BBC.

Pentagon imethibitisha kuwa wanajeshi ni miongoni mwa wale waliouawa - maafisa 11 wa kikosi maalum cha jeshi la Marekani na daktari wa jele wa majini.

Shambulio hilo lilitokea saa kadhaa baada ya serikali za Magharibi kuonya raia kuepuka uwanja huo , kwa sababu ya uwezekano mkubwa wa shambulio kutoka kwa IS-K, kitengo cha Afghanistan cha kundi la Islamic State.

Hapa ndio tunayojua kuhusu kile kilichotokea.

Mlipuko ulitokea nje ya uwanja wa ndege

Mlipuko wa kwanza ulitokea karibu saa kumi na mbili jioni saa za nyumbani (13:30 GMT), karibu na Hoteli ya Baron Hotel, inayopakana na ua la uwanja wa ndege.

Hotlei hiyo ilikuwa inatumiwa na maafisa wa Uingereza kuratibu mipango ya raia wa Afghanistan wanatarajia kusafiri Uingereza.

Ilifuatiwa na makabiliano ya risasi kisha mlipuko wa pili ukatokea katibu na lango la Abbey Gate, moja ya njia kuu ya kuingia uwanja wa ndege.

Ripoti zinasema mlipuko wa pili ulitokea karibu na bomba la kupitisha maji taka ambapo raia wa Afghanistana walikuwa wanasubiri kupewa huduma ya usafiri karibu tu na lango la kuingia uwanja huo wa ndege, na waathiriwa wengine walipeperushwa na kurushwa majini.

Afisa wa Marekani amesema moja wa washambuliaji alikuwa amejifunga vilipuzi.

Wanajeshi wa Marekani na Uingereza hivi karibuni walipelekwa kulindalango kuu la kuingia uwanja huo wa ndege.

Kulingana na walioshuhudia tukio hilo, mshambuliaji mmoja alipiga risasi katika mkusanyiko wa watu ingawa ripoti zingine zinasema walinzi wa Taliban walipiga risasi angani.

Awali raia wa Marekani waliokuwa maeneo ya karibu na uwanja wa ndege walionywa juu ya uwezekano wa kutokea kwa shambulio na kuombwa waondoke "mara moja".

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Uingereza wakilinda Hoteli ya Baron muda mfupi baada ya mlipuko

Idadi ya waliojeruhiwa

Imekuwa ikiongezeka kila siku.

Idadi kamili ya Wamarekani na Waafghanistan - wakiwemo Taliban - waliojeruhiwa bado haijathibitishwa.

Lakini Pentagon imesmea wafanyakazi 12 wa jeshi la Marekani walikuwa wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa. Afisa mwandamizi wa afya huko Kabul aliambia BBC kuwa watu wasiopungua 60 wamekufa, na 140 wamejeruhiwa.

Picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha watu waliojeruhiwa wakieondolewa katika eneo la tukio kwa kutumia mikokoteni

Mikusanyiko mikubwa ya watu imeshuhudiwa katika eneo hilo, wakitumakupata ndehe ya kuondoka nchini humo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Moshi ulionekana ukitanda kote mji mara tu baada ya milipuko hiyo

Baadhi ya nchi tayari zilikuwa zimekomesha shuguli za kuwaondoa watu

Shambulio hili huenda likavuruga shughuli ya kuwaondoa maelfu ya watu Afghanistan.

Kabla ya shambulio, nchi kadhaa ikiwemo Ujerumani, Uholanzi na Canada zilikuwa zimetangaza hazitaendelea na shughuli ya kuwasafirisha watu.

Uturuki imetangaza kuwa wanajeshi wake ambao wamekuwa wakitoa ulinzi katika uwanja wa ndege kwa miaka sita wanaondoka.