Afghanistan: Ngome za ugaidi zinaweza kuzuiwa vipi na nchi za magharibi ?

Afghan commandos forces take part in an operations against the Taliban, IS and other insurgent groups in Achin district of Nangarhar province

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nchi za magharibi , hadi sasa vina usaidizi kutoka kwa vikosi maalumuvya Afghanistan dhidi ya makundi ya uasi nchini humo

"Uingereza itapigana na Islamic State kwa mbinu zozote ziliopo," anasema Dominic Raab. Waziri wa mambo ya nje aliongeza kuwa Uingereza "itakusanya nguvu zote za taifa "kuwasaka viongozi wa kundi hilo

Kwahiyo kauli hii ina maana gani kwa vitendo? Uingereza ina zana gani zilizopo? au hii , kama baadhi ya wakosoaji wanaweza kusema, ni majigambo matupu?

Kwanza , ngoja tutazame nini kilichopotea

Kuchukuliwa kwa karibu nchi yote ya Afghanistan na Taliban inamaanisha kwamba nchi za magharibi-na hususani CIA, MI6 na mashirika mengine ya ujasusi-hazina tena huduma za usalama za kuaminiwa nchini humo au vikosi vya usalama vya Afghanistan vya kushirikiana navyo.

Kwa karibu miaka 20 ambayo Muungano wa NATO na vikosi vngine vya mataifa mbali mbali vimekuwa Afghanistan , ujasusi uliotolewa na makao makuu ya usalama ya taifa umekuwa muhimu katika kufichua shughuli za siri za al-Qaeda, ISIS-K (kikundi cha Afghanistan chenye uhusiano na kundi la Islamic State na makundi mengine ya wanamgambo ya jihadi.

Afghanistan, Marekani, Uingereza na vikosi vingine maalumuwakati huo viliweza kuingia haraka, mara kwa mara kwa helikopta usiku wa manane, na kufunga ngome hizo kabla ya makundi haya kufanikiwa kufanya mashambulio dhidi ya kimataifa.

Japokuwa kuna madai kuwa kwa miaka 20 halijawahi kufanyika shambulio hata moja la kimataifa kutoka Afghanistan, wakati vikosi vya kimataifa vilipokuwa pale.

Kwa hiyo ni nini kimebaki?

Kupoteza ngome zake za Afghanistan na na mifumo iliyoanzishwa ya wapelelezi waliokuwa wakiwapatia taarifa kumeyalazimissha mataifa ya magharibi - hususan Marekani na uingereza- kutegemea sasa mbinu mbili : kuingilia jumbe kwa njia ya mtandao , na njia ya mahsambulio ya njia ya droni.

Ukweli kwamba Marekani haikuweza kuyagundua na kuyashambulia maeneo ya kikundi cha ISIS-K - tawi la IS la Afghanstan lililopo katika Nangarhar haraka sana baada ya shambulio la bomu lililowaua watu Alhamisi wiki iliyopita katika uwanja wa ndege wa Kabul inaonesha kwamba bado kuna tatizo- kwamba haijui kabisa ni nini maadui zake wanapanga katika maeneo ya mbali zaidi ya nchi yasiyoweza kufikiwa kwa urahisi.

Ngome kuu ya jeshi la anga ya Marekani ya Al Udeid - Qatar inaendelea kusimamia operesheni nchini Afghanistan, na wakati eneo la mashambulio linapobaini inaweza kupigia "mitambo " iliyopo katika kanda hiyo na kuviamuru kulishambulia , hususani droni za makombora ambazo zina uwezo wa kupita, bila kuonekana, juu ya eneo kwa saa kadhaa hadi kufikia eneo lililolengwa.

Lakini hauwezi kukwepa ukweli kwamba Afghanistan sasa imekuwa eneo gumu kwa mashirika ya ujasusi. Wengi wa wale watu waliokuwa wakitoa habari kwa mashirika hayo ama wametoroka nchi au wamekwenda mafichoni.

Kituo cha kusikiliza taarifa za upelelelezi cha MI6 na serikali ya Uingereza GCHQ kwa pamoja huripoti kwa waziri wa mambo ya nje , kwahiyo Dominic Raab atakuwa anafahamu vyema changamoto inayomkabili kwa siku zijazo.

GCHQ, pamoja na Shirika la taifa la upelelezi la Marekani kwa pamoja, yamekuwa mashirika ambayo yamekuwa muhimu katika kutambua matawi ya ugaidi ya ISIS katika maeneo kama vile Syria na Iraq.

Lakini ukweli hali ni kwamba MI6 itahitaji kujenga upya mtandao wake wa binadamu wanaoipasha habari za ujasusi iwapo itahitaji kufanikiwa kuwaweka mahali wahudumu wake ndani ya mashirka ya ugaidi nchini Afghanistan ambao wanaweza kutoa tahadhari kwamba shambulio linapangwa. Na hilo linaweza kuchukua miaka.

Hili linaibua swali lingine : je utawahi kuwepo ushirikiano wa kijasusi kati ya taliban na mataifa ya Magharibi?

Ndio, ni jibu,ingawa utakuwa mdogo na pande mbili huenda zisiseme mengi kuhusu ushirikiano huu wazi.

Ni moja ya mambo ya ajabu yasiyo ya kawaida kwa Afghanistan nzima kwamba marekani na Taliban, ambao wamepigana kwa miaka 20 iliyopita, sasa wanajipata kwenye ukurasa mmoja wanapojaribu kukabiliana na ISIS-K.

ISIS-K imetangazwa kuwa adui wa Taliban na al-Qaeda na huenda ikawa kikundi kipya cha uasi kitakachowapa changamoto watawala wpya wa Afghanistan.

Lakini inapokuja kwa al-Qaeda, hali inawa ngumu zaidi.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa mataifa iliyochapishwa mwezi Juni bado kuna uhusiano imara wa kikabila na kindoa baina ya Taliban na al-Qaeda.

Taarifa ya kurejea nchini Afghanistan wiki hii kwa Mshauri mkuu wa zamani wa usalama wa Osama Bin Laden Amin ul-Haq ni ishara inayotisha. Kwamba mtu wa cheo cha thamani ya juu, anayetambuliwa na Marekani kama gaidi mkuu wa kimataifa, anaweza kujihisi kuwa na usalama wa kutosha kurejea kwasababu sasa Marekani imeondoka ni jambo litakalowasumbua maafisa wanaoongoza mapambano dhidi ya ugaidi kaytka nchi nyingi.

Hawataondoa macho yao Afghanistan kwa miaka mingi ijayo..