Nilikuwa na baiskeli kuukuu, bunduki ya zamani sasa ninamiliki silaha za kisasa-Mfuasi wa Taliban

Taliban

Chanzo cha picha, Reuters

Utulivu mkubwa unaonekana katika barabara za Kabul. Inaonekana kwamba asilimia 70 ya magari ya jiji yameondoka mara moja.

Kuna utulivu pia katika viwanja vya ndege, lakini wahudumu wa ndege wa Qatar wamekuja hapa kufanya kazi.

Afisa wa kampuni alisema: "Tunafikiria kufungua uwanja wa ndege haraka iwezekanavyo, kwa siku chache. Kwanza tutajaribu ndege mbili na kisha kuanza safari za ndani na za kimataifa."

Lakini hakuna mtu anayejua itachukua muda gani kuunda serikali nchini Afghanistan.

Katika mahojiano na mwandishi wa BBC, mfuasi wa Taliban anazungumza kuhusu maisha yake.

Mwandishi anasema: Ilitokea wakati tunakula kwenye hoteli, na mara moja mfuasi wa Taliban alivuta kiti kitupu mbele yetu na kuketi. Alikuwa karibu na miaka 25.

Alipokaa chini alituuliza, "mko sawa? Hakuna shida."

Marafiki zangu na mimi tulijibu, "Ndio, kila kitu ni sawa." Aliendelea, "Tumekuja hapa tu kukuhudumia. Vita vyetu vimeisha na sasa kuna amani."

Alijitambulisha kama mshiriki wa 'Makomando' ambao walisemekana kuwa sehemu ya kikundi cha huduma maalum za Taliban. Inasemekana kuwa askari wako kila mahali nchini wakati huo huo wakitoa mafunzo.

Chanzo cha picha, Reuters

Mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana na mfuasi wa Taliban

Kawaida tunakutana na Taliban katika hoteli au nje ya uwanja wa ndege au njiani tukiwa tunakwenda kazini jijini, lakini hii ni mara ya kwanza sisi kuketi ana kwa ana na mkazi.

Wakati mtu huyo wa Taliban alituuliza juu ya hali yetu na wapi tumetoka, tunafanya nini na kadhalika, pia tuliuliza maswali.

Unatoka wapi, umekuwa vitani kwa muda gani? Alijibu, "Nina umri wa miaka 25 na nilikuwa Afghanistan kwa miaka 11. Nilizaliwa nchini Pakistan, ambako nilisoma shule ya Qur'ani."

Aliongeza kuwa vikosi vya Afghanistan havikuacha mapigano. "Walipigana sana. Lakini basi walituonesha picha na video za wanajeshi waliojisalimisha na walituambia jinsi waziri mkuu alivyojisalimisha na vikosi vya Afghanistan pia vilivyojisalimisha.

Chanzo cha picha, Reuters

'Vita ilipoa baada ya kukoma kwa mashambulizi ya anga ya Marekani'

Aliongeza, "Ukamataji unaouona hapa haukutokea kwa urahisi. Tulipambana sana dhidi ya vikosi vya Afghanistan, lakini wakati mashambulio ya angani ya Marekani yaliposimama, ikawa rahisi kwetu kupambana."

Alisema ISIS ilikuwa inasaidiwa. Alisema, "Marekani ilikuwa ikitushambulia, lakini katika eneo hilo hilo wakati ISIS ilipokuwa ikipigana nasi."

Nilipomuuliza alikuwa akipigana wapi na alikuwa akiishi wapi kwa miaka 13 iliyopita, jinsi alivyoishi, alituambia kwamba alikuwa akiishi Kabul na miji mingine ambayo alikuwa amejificha. "Nilikuwa na ndevu fupi. Wakati mwingine tuliishi msikitini na wakati mwingine kwenye madrasa."

Mtu huyo alikuwa mkazi wa mkoa wa Logar. Aliniambia alikuwa amejeruhiwa vibaya mara tano na alikuwa amejaribu mara tatu kutekeleza mashambulio ya kujitoa muhanga dhidi ya Wamarekani.

Mwanamgambo wa Taliban alisema alikuwa kwenye orodha ya wanaotafutwa ya NDS (zamani shirika la ujasusi la Afghanistan) Logar. Baada ya uvamizi wa Taliban nchini Afghanistan, aliona picha zake katika ofisi ya NDS.

'Hatuchukui fedha kwa ajili ya vita'

Alituambia angeweza kutengeneza mavazi ya kujitoa muhanga, kutega mabomu ya ardhini, mabomu ya gari, chochote. Wakati alikuwa akiongea nasi alikuwa akituonesha picha kila mara kwenye simu yake.

Aliongeza, "Hatuchukui pesa kupigana. Nilikuwa nikifanya kazi kwenye shamba la limao na kulipia jihadi."

Alisema alitaka kwenda Palestina, hata ikiwa angeweza kutembea. Alituambia kwamba walitembea hata kwa saa kadhaa wakiwa wamejeruhiwa, na hawakupata bandeji kwa siku kadhaa.

Alisema Wataliban sasa wamepata silaha mpya. "Tuna silaha nyingi. Tuna magari na vifaru. Kuna vitu vingi sana ambavyo huwezi kufikiria."

"Hapo awali, ikiwa nilitaka kushambulia kizuizi, nilikuwa na baiskeli ya zamani na bunduki ya zamani ya C-Kalashnikov. Lakini sasa nina gari, simu. Lakini situmii mwenyewe."

Nikamuuliza ikiwa ameoa. Alijibu, "Zamani tulikuwa tunaenda kwa familia kwa siri, lakini sasa wanafamilia wanataka nioe."