Ndoa za utotoni: 'Niliolewa kwa lazima usiku, sikusema chochote kwasababu wangeniua'

Chanzo cha picha, Getty Images
Priyanka mwenye umri wa miaka, 11, aliolewa mnamo mwezi Mei mwaka huu.
Dada zake wote wanne walikuwa wameolewa wakiwa na umri mdogo, Priyanka alikuwa akituambia.
Alikuwa akiishi na dada yake kwa miaka miwili iliyopita akihofia kuwa pia naye, sio mbali, atakuwa mwathirika wa ndoa ya utotoni.
"Dada yangu ananipenda sana. Nilimwambia sitaki kuolewa badala yake nataka kukaa tu na naye. Nilikuwa nikimtunza mtoto wake mdogo wa kiume huko na kwenda msituni kulisha kondoo na mbuzi," Priyanka alikuwa akizungumzia undugu wake.
Kwa bahati mbaya, Priyanka, alisoma kigogo tu na baada ya hapo hakuendelea tena na msomo.
Riziki ya familia yake inategemea kazi ngumu.
Kiangazi kibaya kilianza katika eneo lililokumbwa na ukame mbaya.
Kabla ya Priyanka kwenda msituni, baba yake walikuja na gari na kumpeleka kijijini kwa mjomba wake.
'Ningepigwa kama dada yangu ...'
"Sikujua nini kitatokea baadaye. Niliamka nyumbani kwa mjomba wangu mchana ule. Chakula aina ya wali ulikuwa unaandaliwa. Mbali na dada yangu mdogo, wengine wakubwa wanne hakuna aliyekuwepo hata mmoja.
Kulikuwa na watu wachache sana. Wakati wa jioni, mama yangu na mjomba walinipa sari nyekundu nivae. Nikavaa vito vya mapambo mikononi, shingoni na miguuni.
Ilikuwa usiku na sikujua chochote kinachoendelea. Kwanini sikuuliza swali lolote? Ikiwa ningeuliza, Ninajua kabisa kwamba baba yangu angenipiga kama alivyomfanya dada yangu. Niliolewa kwa nguvu."
Chanzo cha picha, Getty Images
"Uliolewa vipi? Alipoulizwa swali hili, Priyanka alianza kuchanganyikiwa, na kuonyesha hofu kwenye uso wake.
Tulimuuliza swali hili mara mbili au tatu.
Lakini aliepuka kulizungumzia.
Ila alisema kitu kimoja.
Baba alichukua pesa kutoka kwa aliyekuwa mume wake ambaye alilipia harusi.
Hakujua ni pesa ngapi zilizochukuliwa.
Lakini alisisitiza- "Nusu imechukuliwa na nusu ikaachwa kwa ajili ya kutolewa kwa wazee."
Baada ya ndoa hii ya utotoni, mama mkwe wa Priyanka alifariki dunia lakini baadaye msichana huyo mdogo akaokolewa katika ndoa hiyo na kuchukuliwa na Kamati ya Ustawi wa Watoto ya Wilaya kwa msaada wa polisi kuanzia mnamo mwezi Julai 26.
Imebainika kuwa Navradeva ana umri wa miaka 28.
Chanzo cha picha, Getty Images
Polisi wa vijijini wanachunguza zaidi ikiwa Priyanka alikuwa alisafirishwa kwa njia haramu kuingizwa kwenye ndoa hiyo ya utotoni.
Kamati nyingi za ustawi wa watoto wilayani zinasema kwamba idadi ya visa kama hivyo vya ndoa za utotoni vimeongezeka wakati wa kufungiwa ndani kudhibiti ugonjwa wa virusi vya corona.
Priyanka hajui kwamba ametendewa isivyo haki.
Priyanka anasema, "Wakati dada zangu walipoolewa, walikuwa tayari wameanza kupata hedhi, lakini mimi bado sikuwa nimeanza kupata hedhi."
'Unawezaje kuelezea hisia zako?'
Kwa sasa, Priyanka anakaa katika taasisi hadi uchunguzi wa polisi utakapokamilika.
Anataka kwenda nyumbani.
Lakini hawezi kukuambia haswa ni wapi unaweza kujisikia yuko salama.
Priyanka hana lugha ya kuelezea anachofikiria, anahisije au anachotaka.
Tuliomba msaada wa mkalimani ambaye alizungumza lugha yake ili kujua nini kilikuwa kikiendelea akilini mwake.
"Sikutaka kuolewa," alisema.
'Kufanya mapenzi katika ndoa ya utotoni ni sawa na kutekeleza vurugu'
Ndoa ya utotoni ina athari kubwa kwa afya ya wasichana.
Kuanza kushiriki ngono katika umri mdogo, kuna hatarisha msichana kupata ujauzito.
Pia kulingana na Nandita Shah, mwanzilishi mwenza wa Kituo cha sheria, hali hii ya vurugu ya ndoa za utotoni hadi miaka 18 ni sawa na ubakaji.
Na kituo chake, kimekuwa kikifanya kazi kwa uwezeshaji wa wanawake na wasichana tangu 1995 na kusaidia wasichana vijana kukuza ujuzi wao ili waweze kujisimamia kimaisha.
Chanzo cha picha, Getty Images
Athari ya kufanya mapenzi na mtoto mdogo
Daktari wa wanawake anayefanya kazi katika maeneo ya vijijini anazungumza juu ya athari ya ndoa za utotoni kimwili na kiakili kwa wasichana.
Aishwarya Revadkar anasema, "Wavulana na wasichana ambao wamebalehe wanapitia ukuaji wa mwili, mabadiliko ya homoni, ukuaji wa sehemu zao za siri, kukomaa na mabadiliko ya akili. Kuwa katika ndoa kipindi hicho sio tu kwamba kunaathiri msichana, lakini pia mwili wake."
Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa kuongezea, kwasababu ya ukosefu wa ufahamu juu ya uzazi wa mpango, msichana anakuwa mjamzito katika miezi michache tu.
Mwili wake ambao haujakomaa hauko tayari kwa ujauzito na kwasababu ya ujauzito wa mapema, wasichana wanakabiliwa na upungufu wa damu, shinikizo la juu la damu na hata kujifungua kwa njia ya upasuaji.
Pia, wasichana hawa hujifungua kabla ya miezi tisa na wanazaa mtoto mwenye uzito mdogo.
Mchakato mzima ni hatarishi kwa mwili wa msichana, na pia hupitia tatizo la kiakili na wasichana hufikia utu uzima wa mapema.
Pia, moja ya sababu nyingi za saratani ya kizazi ni kuanza kushiriki ngono mapema kutokana na ndoa za utotoni.
'Sehemu nzuri ya kuzungumzia unachofikiria'
Kipindi cha Covid kimeathiri mapato na biashara ya familia nyingi.
Wazee wa familia walianza kumfikiria Ozhan kama msichana ambaye amekomaa kwasababu ya ukosefu wa mapato katika familia masikini.
Uchumi ni moja ya sababu kuu inayochangia ndoa za utotoni.
Na pigo kubwa kipindi hiki limekuwa ukosefu wa ajira kwa wengi.
Sasa kwasababu ya corona, idadi ndogo tu ya watu ndio wanaalikwa kwenye harusi na kuwezesha tabia ya kupitisha ndoa hizo za utotoni kisiri.
Chanzo cha picha, Getty Images
Kutoroka nyumbani kwa hofu ya ndoa ya utotoni
Mama yangu alifariki dunia nilipokuwa mtoto, baba yangu na bibi walikuwa nyumbani, na ilikuwa vigumu kumtunza Renuka akiwa mdogo.
Kwa hivyo, Renuka alianza kusoma akiwa anaishi ndani ya shule ya serikali.
Mwaka wa kumi ulikuwa muhimu sana kwa Renuka, lakini ilani ya kutotoka nje ikaanza kutekelezwa mwezi huo huo, mnamo Machi 2020, Renuka alirudishwa nyumbani.
Maisha yake ya kila siku yalibadilika ghafla.
Renuka alikuwa na hakika kwamba elimu ingeboresha maisha yake.
Lakini aliporudi nyumbani, ghafla, baba yake aliamua kumuoza.
Renuka wa miaka 15, ambaye haki yake ilikandamizwa, alitoroka nyumbani asubuhi na mapema na kutembea kilomita 17 hadi kituo cha polisi na kurudishwa katika shule ya serikali kutokana na agizo la polisi.
Visa hivi ni baadhi tu vinavyonesha jinsi wasichana wenye umri mdogo wanavyotaabika kwa kulazimishwa kuingia kwenye ndoa za utoto bila hata wao wenyewe kujua.
Na mbaya zaidi, ni wazi kwamba visa hivi vimeongezeka zaidi siku za hivi karibuni kutokana na athari ya ugonjwa wa corona na kusababisha wengi kukatiza masomo yao.