Maisha katika nyuzijoto 50: Athari za mabadiliko ya hali ya hewa ,ndani ya maisha ya Waaustralia
Maisha katika nyuzijoto 50: Athari za mabadiliko ya hali ya hewa ,ndani ya maisha ya Waaustralia
Australia ni mojawapo ya nchi ambazo tayari zinashuhudia ongezeko kubwa la idadi ya siku za joto kali kupindukia, huku maeneo kama Sydney yakishuhudia viwango vya joto vya karibu nyuzijoto 50. Ukali wa joto umesababisha kuibuka kwa visa vya moto ya msituni, huku baadhi ya makundi ya spishi asilia wakifariki.

Mabadiliko ya tabia nchi : Sasa dunia inashuhudia mara dufu idadi ya siku ambazo nyuzijoto ni zaidi ya 50
Utafiti wa BBC umebaini kuwa siku zenye nyuzijoto zaidi ya 50 zimeongezeka mara mbili katika kipindi cha miaka 40 iliyopita.