Afghanistan: Fahamu makampuni makubwa ya Marekani yaliojitajirisha na vita vya taifa hilo

Kwa kila mwanajeshi mmoja wa Marekani kulikuwa na wanakandarasi wawili

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kwa kila mwanajeshi mmoja wa Marekani kulikuwa na wanakandarasi wawili

Ilikuwa vita ya muda mrefu zaidi katika historia ya Marekani, lakini moja kati ya vita zilizogharimu mapesa mengi.

Vita vya Afghanistan, vilivyohitimishwa Agosti 30 mwaka huu baada ya vikosi vya Marekani kuondoka Kabul, imeigharimu Marekani dola bilioni $ 2.3 billion, kwa mujibu wa Chuo kikuu cha Brown huko kisiwani Rhode.

Kurejea madarakani kwa kundi la Taliban nchini Afghanistan na kuondoka kwa vikosi vya Marekani nchini humo kunaonekana na wachambuzi wengi kama ishara ya kwamba ni vita ambayo haikuwa na mafanikio.

Kwa wengi inaonekana kama vita isiyo na mafanikio, lakini kwa wengine ilikuwa fursa ya kutengeneza faida kubwa.

Kati ya dola trilioni $2.3 zilizotumika kwenye vita hiyo kati ya mwaka 2001 na 2021, karibu dola trilioni $1.05 zilienda kusaidia matumizi na shughuli za uendeshaji wa kitengo cha ulinzi cha Marekani huko Afghanistan.

Sehemu kubwa ya fedha hizo zilitumika kulipia huduma za makampuni binafsi ambayo yaliunga mkono operesheni za Marekani nchini Afghanistan.

"Vita hivyo vilikuwa na vikosi vidogo sana vya Marekani - wote wanaojitolea - waliongezwa kama wakandarasi wa kijeshi. Kwa ujumla, kulikuwa na wafanyakazi mara mbili ya wanajeshi wa Marekani," anasema Linda Bilmes, profesa kutoka Chuo Kikuu cha Harvard.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Makampuni yaliopatiwa kandarasi yalitoa huduma tofauti kutoka kufanya usafi , kupikia wanajeshi na kuhakikisha vifaa vya kijeshi vya Marekani vilikuwa katika hali nzuri

"Kwa sababu ya uwepo wa kazi nyingi za kufanywa, ilimaanisha wafanyakazi wengine kusaidia kuweka mafuta kwenye ndege, kuendesha magari makubwa, kupika, kusafisha, kuendesha helkopta na kusafirrisha vitu mbalimbali. Wengine walitumika kujenga makambi ya kijeshi, viwanja vidogo vya dege na njia za ndege.", aliongeza.

Makampuni matano yaliyolipwa pesa nyingi

Mamia ya makampuni kutoka Marekani na nje ya Marekani yalipata mikataba ya kufanya kazi na Jeshi la Marekani kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa jeshi hilo nchini Afghanistan, kati ya hao yapo yaliyolipwa mabilioni ya dola.

Ingawa hakuna orodha inayoonyesha makampuni gani yamelipwa zaidi, Profesa Heidi Peltier, kutoka chuo kikuu cha Boston - anaiambia BBC makadirio yake. Makadirio haya ni pamoja na taarifa zinazopatikana kwenye tovuti ya serikali

Chanzo cha picha, Getty Images

Kampuni zilizokuwa na kandarasi kubwa nchini Afghnaistan

•$14.4 billion Dyncorp International

•$13.5 billion Fluor Corporation

•$3.6 billion Kellogg Brown Root (KBR)

•$2.5 billion Raytheon Technologies

•$1.2 billion Aegis LLC

"Takwimu hizi ni za kipindi kati ya mwaka 2008-2021, ingawa mikataba mingine iliyojumlishwa huenda ikawa ni ya nyuma ya mwaka 2008, kwa hivyo takwimu sahihi inaweza kuwa zaidi ya hizo kama tukiwa na taarifa zote za toka mwaka 2001.

Kwa mujibu wa makadirio yao, makampuni matatu ya Marekani yaliyopata mikataba minono nchini Afghanistan yalikuwa ni Dyncorp, Fluor, na Kellogg Brown and Root (KBR).

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kampuni ya Dyncorp ilikuwa na wajibu wa kumlinda Rais wa Afghanistan wakati huo Hamid Karzai.

Kwa mujibu wa Peltier, Dyncorp — ilipata mkataba wenye thamani ya dola bilioni $14.4.

"Tangu mwaka 2002, Dyncorp imekuwa ikifanya kazi bega kwa began a serikali na washirika wake nchini Afghanistan. Tukitoa huduma mbalimbali," alisema msemaji wa kampuni hiyo aliiambia BBC.

Aliongeza kwa sababu ni kampuni binafsi hawawezi kutoa maelezo zaidi ya mkataba wao na Jeshi la Marekani ulikuwaje na fedha kiasi gani walipata.

Fluor, Kampuni yenye makazi yake Texas, ilikuwa na jukumu la kujenga kambi za jeshi la Marekani Kusini mwa Afghanistan.

Kwa mujibu wa tovuti ya kampuni hiyo ilishiriki kusaidia zaidi ya wanajeshi 100,000 na kuhudumia kwa kutoa vyakula vya watu zaidi ya 191,000 kwa siku.

Kwa ujumla, Fluor Corporation ilipata mkataba wenye thamani ya dola bilioni $13.5

BBC Mundo iliiomba Fluor kuhusu shughuli zake wakati wa vita nchini Afghanistan, lakini mpaka wakati wa kuchapisha Makala haya, BBC haikuwa imepata ajibu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kampuni ya Fluor Corporation imekuwa ikitoa huduma mbalimbali kwenye kusaidia operesheni kwenye makambi ya kijeshi ya Marekani.

Kellogg Brown Root (KBR), kwa upande wake ilikuwa ikihusika na masuala ya uhandisi na vifaa kusaidia vikosi vya Marekani kwenye upande wa malazi, chakula na huduma zingine za msingi

Kwa mujibu wa makadirio ya Peltier, KBR ilipaa mkataba unaofikia thamani ya dola bilioni $3.6 billion.

Kampuni ya nne ilikuwa ni Raytheon, moja ya makampuni makubwa ya Moja ya makampuni makubwa zaidi ya masuala ya anga na ulinzi za Marekani, ambayo ilishinda zabuni ya dola bilioni 2.5.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Moja ya kazi yake kubwa ya hivi karibuni ilikuwa ni kufundisha jeshi la anga la Afghanistan, kazi ambayo walilipwa dola milioni $145 katika zabuni walioshinda mwaka 2020.

Aegis LLC,a kampuni ya ulinzi yenye makazi yake Virginia ilikuwa kampuni ya tano kwa makampuni yaliyolipwa fedha nyingi wenye operesheni za kivita Afghanistan, ikipata mkataba wenye thamani ya dola bilioni $1.2.

Moja ya majukumu yake makubw ailikuwa ni kutoa huduma za ulinzi kwa ubalozi wa Marekani katika mji wa Kabul.

BBC Mundo pia iliwasiliana nao kuuliza kuhusu majukumu yao, lakini mpaka tunachapisha taarifa hii, hawakuwa wamejibu.

Vipi kuhusu makampuni ya Ulinzi?

Wataalam wameieleza BBC kwamba wanakubaliana ya kuwamba makampuni makubwa ya ulinzi Marekani kama Boeing, Raytheon, Lockheed Martin, General Dynamics na Northrop Grumman nayo yalinufaika pakubwa na vita vya Afghanistan.

"Yametengeneza hela nyingi kutokana na vita,"anasema Linda Bilmes.

0ata hivyo ni vigumu kubainisha ni kiasi gani cha pesa zimepata kampuni hizo kwa sababu hazikuwa zinahusika moja kwa moja na shughuli za oparesheni nchini Afghanistan.

"Yote yalipata mikataba kutengeza vitu ambavyo vilikuwa vinatumika na Marekani nchini Afghanistan," Peltier says.

Inaelezwa kuwa kati ya mwaka wa fedha wa 2001-2020, makapuni haya kwa pamoja yaliingiza dola trilioni $2.1.

BBC Mundo pia ilituma maombi kwa makampuni haya kujua kwa namna gani vita vya Afghanistan vimewanufaisha, lakini haikupata majibu mpaka wakati wa kuchapishwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kwa mujibu wa Peltier, kampuni ya Raytheon ilijipatia mkataba wa dola milioni $ 2.5. Kampuni hiyo ya masuala ya teknolojia ya anga ilihusika kutoa silaha, mifumo ya mawasiliano na huduma zingine.

Boeing pia ilitengeneza ndege aina ya F-15 na F-18 fighter ambayo Linda Bilmes anailelezea kama ndizo zilikuwa muhimu katika operesheni za kijeshi za Marekani nchini Afghanistan.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Lakini Boeing haikuwekwa kwenye orodha ya makampuni yaliyopata mikataba minono wala Lockheed Martin

Lakini Boeing haikuwekwa kwenye orodha ya makampuni yaliyopata mikataba minono wala Lockheed Martin, kampuni nyingine kubwa ya ulinzi nchini arekani, watengenezaji wa helkopta za blackhawk, ambazo zimetumika sana cnhini humo.

Wataalam wanaeleza kuwa makampuni haya ya ulinzi ni makubwa na yametengeza fedha nyingi kwa kufanya vitu ambavyo vingine havikuwa vinatumika moja kwa moja kwenye vita.

Msemaji wa Jeshi la Marekani, Jessica Maxwell ameiambia BBC kwamba ni ngumu kusema kiwango gani cha pesa makampuni haya matano makubwa ya ulinzi yamepata kwa ajili ya vifaa na huduma zao zilizotumika kwenye vita nchini Afghanistan.

"Ni ngumu kupata makadirio hayo," alisema.

Bei zisizo za ushindani

Bilmes anagusia jambo linginewakati wa vita nchini Afghanistan kwamba wazabuni walikuwa na haki ya kuweka bei wanayoiona inafaa kwa huduma zao.

"Mikataba mingi ilitolewa bila ushindani au kwa ushindani mdogo mno. Hii ni kwa sababu kuna wakati mtoa huduma ni mmoja tu, lakini pia hakukuwa na makampuni mengi makubwa yaliyokuwa yanaweza kufanya kazi tuliyokuwa tunaitaka. Kwa hivyo walitaja bei ambayo walioitaka.

"Sera ya Idara ya ulinzi ilikuwa ni kutoa kazi kwa kushindanisha wazabuni. Ingawa mifumo mingi ya silaha iliwekwa kwenye zabuni lakini ukweli, mara nyingi unakuta ni kampuni moja tu inayozalisha," aliongeza Bilmes.

Kunatajwa pia mabilioni ya dola, yamekwapuliwa kwa njia ya rushwa wakati wa zoezi hili la vita na kuna wakati bei ya vitu iliwekwa juu kwa makusudi.

"Kuna wakati unaweza kupiga rangi jengo lakini ukalipwa mara 20 ya gharama halisi . Kulikuwa na rushwa na hiyo naweza kuita bajeti hewa," alisema

Gazeti na New York Times, liliwahi kuripoti kuwa kati ya mwaka 2008 na 2017, ofisi ya ulinzi ya Marekani iliripoti ubadhirifu wa dola bilioni $15.5 zilizodaiwa kutumika vibaya wakati wa wa juhudi za kuijenga upya Afghanistan.