Aukus: China inachukizwa na nini katika mkataba kati ya Marekani, Uingereza na Australia?

China imeukosoa mkataba wa usalama wa kihistoria 'Aukus' uliosainiwa na chi za Marekani, Uingereza na Australia, ikiita kitendo hicho ni kutowajibika

Chanzo cha picha, Getty Images

China imeukosoa mkataba wa usalama wa kihistoria 'Aukus' uliosainiwa na chi za Marekani, Uingereza na Australia, ikiita kitendo hicho ni kutowajibika. China inasema mkataba huo ni mfano wa fikra ndogo.

China imelaani makubaliano hayo ya ulinzi kati ya Marekani na Australia, ikisema yanaakisi "fikra za vita baridi". Uingereza, Marekani na Australia zimetangaza kuingia kwenye makubaliano maalumu ya masuala ya usalama.

Chini ya makubaliano hayo, Marekani pia itatoa teknolojia ya nyuklia kwa Australia. Wataalamu wanaamini kuwa makubaliano hayo mapya ya usalama yamelenga kukabiliana na ushawishi wa China huko eneo la Asia Pasifiki.

Eneo hili limekuwa chanzo cha utata na mivutano mingi inayoendelea huko. "Hizi ndizo sababu za juhudi za kuzuia kuenea kwa silaha za kimataifa zinaonekana kuwa za kushangaza," anasema Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian.

Waziri huyo amelaani makubaliano hayo mapya ya ulinzi kati ya Marekani, Uingereza na Australia, akisema yanaakisi "mawazo ya vita baridi". Vyombo vya habari vya serikali ya China vimechapisha pia kolamu za wahariri kulaani makubaliano hayo.

Kwa makubaliano haya, Australia imejiweka yenyewe kwenye upande wa kuipinga China, kwa mujibu wa Makala iliyochapishwa na Global Times.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa mara ya kwanza katika miaka 50 Marekani inashirikisha teknolojia yake ya manowari za nyuklia.

Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 50 ambapo Marekani inashirikiana nan chi tofauti kwenye teknolojia yake ya manowari. Awali Marekani ilikuwa inashikiriana kwenye teknolojia hiyo na nchi ya Uingereza pekee.

Hatua ya sasa inamaanisha kwamba Australia sasa itakuwa na uwezo wa kutengeneza manowari zake za nyuklia ambazoo itakuwa na kasi zaidi kuliko manowari ya kawaida. Manowari hizi maalum zinaweza kukaa chini ya maji kwa miezi kadhaa zikiwa na uwezo wa kufyatua makombora kwa kwa masafa marefu.

Awali, Rais wa Marekani Joe Biden, Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison walieleza kwa ufupi kuhusu makubaliano hayo katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

Ingawa katika mkutano huo hakuna kati yao aliyeitaja China moja kwa moja, lakini viongozi hao wote watatu waliwahi kuzgusia wasiwasi wao kuhusu usalama katika ukanda wao.

Katika taarifa yao ya pamoja kuhusu makubaliano hayo ya usalama ilisema, "Katika Mpango huu wa kwanza chini ya Aukus tutahakikisha tunajenga manowari kubwa zinazotumia nyuklia kwa ajili ya Jeshi la majini la Australia."

Chanzo cha picha, Getty Images

Nchi gani nyingine zina Manowari za nyuklia?

Wachambuzi wanasema makubaliano hayo ni moja ya makubaliano muhimu zaidi ya usalama yaliyowahi kutiwa saini kati ya nchi hizo tatu baada ya vita vya pili vya dunia.

Kwa ushirikiano huo, Australia sasa itakuwa na Manowari za nyuklia kwa mara ya kwanza kabisa. Hiyo inamaanisha Australia itakuwa nchi ya saba duniani kuwa Manowari za nyuklia.

Awali nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa, China, India na Urusi zimewahi kuwa na teknolojia hiyo. Makubaliano hayo yanahusisha pia masuala ya ujasusi na ushirikiano kwenye masuala ya mtandao.

"Hili linaonyesha dhahiri kwamba nchi hizi tatu zimechukua hatua hii muhimu mapema kukabiliana na tishio lolote," alisema Guy Bokenstein kutoka Jumuia ya wa-Asia nchini Australia.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, alisema makubaliano hayo yatasaidia kudumisha usalama na utulivu duniani kote na pia kuunda "mamia ya ajira."

Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wales ameiambia BBC kuwa kihistoria China imekuwa ikiongeza bajeti kubwa za shughuli za kijeshi, kwa hivyo tunataka washirika wetu katika eneo hilo wasimame kwa miguu yao wenyewe.

Katika miaka ya hivi karibuni, beijing imekuwa ikishutumiwa kwa kuongeza mivutano katika maeneo yanayozozaniwa kama vile bahari ya kusini mwa China.

China inadai kuwa mambo ambayo yanasemwa kuhusu eneo hilo ni haki za muda mrefu, zakarne nyingi na kwamba inachokifanya ni kuongeza majeshi yake katika eneo hilo ili kulinda haki zake.

Marekani pia imeongeza majeshi yake katika eneo hilo na imekuwa ikiwekeza sana kwenye ushirika wake na washirika kama Japan na Korea Kusini. Wachambuzi wanasema kuwa kuwa uwepo wa Manowari nchini Australia ni muhimu katika kuimarisha ushawishi wa Marekani katika eneo hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mvutano kati ya Australia na China waikasirisha Ufaransa

China ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Australia na nchi hizo mbili zimemekuwa na uhusiano mzuri kwa miaka mingi.

Lakini mivutano ya kisiasa katika miaka ya hivi karibuni imesababisha mzozo mkubwa baina ya nchi hizo mbili.

Australia kuikosoa China kwa namna inavyoshughulikia waislamu wa Uighur, marufuku ya Huawei kuhusu matumizi ya baadhi ya na teknojia na Ushiriki wa China kwenye katika janga la virusi vya corona kumesababisha mzozo kati ya nchi hizo mbili.

Mataifa ya Magharibi pia yana wasiwasi mkubwa na uwekezaji wa miundombinu unaofanywa kwa kasi na China hasa katika eneo hilo la Pasifiki.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema Marekani itashirikiana kidete na nchi ya Australia katika ulinzi wake dhidi ya China.

Hata hivyo makubaliano ya sasa unaonekana kama kuigusa Ufaransa iliyoanza kuingia makubaliano na Australia kuhusu Manowari. Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Zo Eve le Dreyan ameielezea hatua hiyo ni kama "kudungwa kisu." Miaka mitano iliyopita Ufaransa ilitia saini makubaliano ya kuiuzia Australia Manowari 12 za kawaida.

Mkataba huo ulikuwa na thamani ya Euro bilioni 56, lakini baadaye ilikuja taarifa habari kwamba Uingereza-Marekani-Australia walikuwa wakiufanyia kazi ushirikiano wa kimkakati.

Umoja wa Ulaya umeelezea kutofurahishwa na makubaliano hayo ya ulinzi ya 'Aukus' yaliyotiwa saini kati ya Marekani, Australia na Uingereza.

Chanzo cha picha, EPA/OLIVIER HOSLET

Umoja wa Ulaya Unasemaje hasa?

Msemaji wa Umoja wa Ulaya Peter Steno ameelezea kushangazwa kwake kwamba hakuna taarifa yoyote rasmi iliyotolewa kwa umoja huo kuhusu mkataba huo na kuongeza nchi wanachama wa Umoja huo watafuatilia athari zake.

Katika hatua nyingine, mwakilishi wa Umoja wa Ulaya katika masuala ya nje na sera za kigeni, Josep Burel, alisema, "tumekuja tu kujua tu juu kuhusu makubaliano haya, hatukulzungumzia hili na Marekani.

'mimi ni mwakilishi mkuu wa umoja kuhusu masuala ya usalama, lakini pia sikujua hilo. Naamini kuwa haya si makubaliano ya ghafla. Inachukua muda kwa makubaliano kama haya kufanyika."

"hatujalizungumza hili awali na nadhani huu ni wakati sahihi wa kufikiri kwamba suala hili linapaswa kuletwa na kujadiliwa katika mamlaka za juu."

Hata hivyo, alisema hatua hiyo inaweza kuimarisha zaidi ushirikiano huo ikiwa nchi wanachama watataka.