Takribani watu milioni 26 wataabika kupata chakula kutokana na ukame

Takribani watu milioni 26 wataabika kupata chakula kutokana na ukame

Takriban watu milioni 26 wanatatizika kupata chakula kufuatia misimu duni ya mvua mfululizo katika Pembe ya Afrika.

Hali ya ukame kaskazini mwa Kenya, sehemu kubwa ya Somalia na Kusini mwa Ethiopia inatabiriwa kuendelea hadi angalau katikati ya mwaka ujao, na kuweka maisha ya watu wengi hatarini.

Tayari hali ni mbaya sana, wanyama pori wanakufa kwa mamia yao na wafugaji wanaripoti hadi 70% ya vifo vya mifugo. Mwandishi wa BBC barani Afrika Anne Soy anaripoti kutoka Wajir kaskazini mwa Kenya.