Bilionea wa Japan asafiri anga za mbali kucheza gofu

Russian cosmonaut Alexander Misurkin (C) and space flight participants - Japanese billionaire Yusaku Maezawa (L) and his assistant Yozo Hirano - attend a training ahead of the expedition to the International Space Station, in Star City outside Moscow on 14 October 2021.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Bilionea wa Kijapani Yusaku Maezawa (kulia) aliandamana na mwanaanga wa Urusi Alexander Misurkin (Kati) na msaidizi wa uzalishaji Yozo Hirano (Kulia)

Mfanyabiashara wa Japan Yusaku Maezawa amesafiri kwenda kituo cha kimataifa cha anga za mbali, kujiunga na orodha ya mabilionea ambao wamezuru anga hizo.

Akiwa huko anapanga kufanya mambo kadhaa, ikiwemo kucheza gofu.

Bw, Maezawa amepata utajiri wake kupitia kampuni za biashara za mtandaoni ikiwemo Zozotown.

Wakati mmoja alikuwa mpiga ngoma jatika bendi ya muziki wa rock, na mwaka jana ilizindua show ya kutafuta rafiki mpya wa kuungana naye angani, lakini baadaye akaghairi.

Roketi ya Kirusi iliyombeba Bw Maezawa ilipaa kutoka eneo la Baikonur Cosmodrome huko Kazakhstan.

Anatarajiwa kuwa angani kwa siku 12 katika kituo cha kimataifa cha anga za mbali (ISS), na ndiye mtalii wa kwanza wa anga kuzuru kituo hicho katika miaka ya hivi karibuni.

Ni kitangulizi cha safari ya Bw Maezawa kwenda mwezini iliyotangazwa sana mwaka wa 2023.

Ziara hiyo ya Jumatano inamuonyesha Bw Maezawa akiandamana na mwanaanga wa Urusi Alexander Misurkin na mtayarishaji wa video Yozo Hirano, ambaye anarekodi safari hiyo kwenye ya chaneli ya YouTube ya bilionea huyo.

Kabla ya kuanza safari hiyo Bw Maezawa alifanya mafunzo maalum, ambayo ni pamoja na kulala kwenye kitanda kilichoegemezwa, kuzungushwa kwenye kiti na kucheza badminton kwa muda mrefu - yote ambayo ameandika kwenye mitandao ya kijamii.

Katika mkutano na waandishi wa habari hapo awali Bw Maezawa alisema safari hiyo ni "ndoto iliyotimia".

"Watu wanaweza kuwa na matumaini na ndoto (kwa kuona kwamba) mtu wa kawaida kama mimi anaweza kwenda katika ulimwengu usiojulikana," alisema bilionea huyo.

Akiwa katika ziara hiyo ameahidi kufanya vitu 100, vilivyotolewa kwenye orodha ya mapendekezo yaliyochangiwa na umma.

Inatofautiana na inavyotarajiwa, kama vile kuwatambulisha wanaanga wenzake na kuwaonyesha watazamaji jinsi maisha yalivyo kwenye anga za mbali; na mengine kama vile kucheza gofu, kupuliza mapovu, na kurusha ndege ya karatasi.

Safari ya Bw Maezawa, ambayo inaripotiwa kumgharimu $88m (£66m), inafuatia safari fupi ya bilionea mwenzake Jeff Bezos kwenda angani na Richard Branson kuelekea ukingo wa anga mapema mwaka huu, katika roketi zilizotengenezwa na makampuni yao ya kibinafsi.

Yusaku Maezawa ni nani?

Mjasiriamali wa Kijapani anayejulikana kwa historia yake ya kipekee. Mpiga ngoma huyo wa zamani wa bendi ya rock ya punk alianzisha kampuni iitwayo Start Today mwaka 1998 akiuza CD na rekodi adimu.

Baadaye alijihusisha na uanamitindo na mchuuzi wa kielektroniki wa Zozotown mnamo 2004, na akawa bilionea alipokuwa na umri wa kati ya miaka 30.

Jarida la Forbes limemworodhesha kuwa tajiri wa 30 wa Japani, akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia $1.9bn (£1.43bn).

Mapenzi ya Bw Maezawa ya kusafiri angani yamenakiliwa vyema katika miaka ya hivi majuzi.

Aligonga vichwa vya habari vya kimataifa mnamo 2019 alipofichuliwa kuwa abiria wa kwanza wa kibinafsi aliyepangwa kuzunguka Mwezi na SpaceX, kampuni inayomilikiwa na bilionea mwenzake Elon Musk.

Safari hiyo ya ndege, inayoitwa dearMoon, imeratibiwa kufanyika mwaka wa 2023. Bw Maezawa alitangaza mwezi Machi kwamba ataandamana na watu wanane na atagharamia safari nzima.

Kwa nini Urusi inampeleka angani?

Siku ya Jumatano Bw. Maezawa alisafiri kwenda angani kwa kutumia roketi ya Urusi ya Soyuz, na ndiye mtalii wa kwanza wa anga za juu aliyejifadhili mwenyewe kusafiri hadi ISS katika zaidi ya muongo mmoja.

Kwa miaka mingi njia pekee ya kufikia ISS ilikuwa kusafiri kwa chombo cha Soyuz, na Urusi ina rekodi ya kuwapeleka watalii wa anga kwenye kituo hicho katika miaka ya 2000 ikiwa ni pamoja na milli ya Marekani.

Ilisimamisha mpango wake wa nafasi ya kibinafsi mnamo 2010.

Lakini kutokana na wazo la utalii wa anga kushika kasi, kwa kiasi fulani lililochochewa na makampuni kama vile SpaceX, imeanza kuruhusu wateja wanaolipa kama Bw Maezawa kwenye uzinduzi wake tena.

Urusi pia ilimpeleka mwelekezaji wa filamu Klim Shipenko na mwigizaji Yulia Peresild kwenye kituo hicho mwezi Oktoba, ambao walirekodi matukio ya filamu ijayo.