Mohamed Salah ndiye bora zaidi bila ya kipindi cha Messi na Ronaldo

Mo Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Kandarasi ya Mohamed Salah huenda isiwe wazi lakini hali ya mchambuliaji huyo kama mmchezaji bora wa nyakati zote haina shaka.

Salah amekuwa katika hali nzuri zaiid msimu huu na bao lake dhidi ya AC Milan katika Champions League siku ya Jumanne lilifikisha mabao 20 katika mashindano yote na bado ni mapema Desemba.

Kwa tarehe, ni mawiji tu wa Liverpool Ian Rush Novemba 7 na Roger Hunt Novemba 25 waliofika kiwango hicho haraka kuliko Salah ambaye pia amesaidia mara tisa

Bila Lionel Messi na Cristiano Ronaldo tunaweza kumfikiria kwa njia gani Mohamed Salah sasa hivi? Aliuliza Pat Nevin katika BBC Radio 5. "Tutamuona kama mchezaji bora zaidi katika soka."

Meneja wa zamani wa Celtic Neil Lennon alisema: "Mohamed Salah yuko pale juu na mchezaji mwingine yeyote nimeona katika miaka michache iliyopia. Ndiye mchezaji nimeona akimkaribia sana Lionel Messi."

'Anaweza kwenda wapi? Soka ya Uhisapania inakubwa na matatizo'

Liverpool walianguka kufutia juhudi za beki Muingereza Fikayo Tomori kwa AC Milan kabla Slah kusawazisha dakika ya 36.

Salah aliitikia kwa haraka jitihada za kipa Mike Maignan kuokoa mkwaju wake Alex Oxlade-Chamberlain.

"Anafikia vitu kwa njia tofauti. Anaonekana kupata nguvu kutoka mguu wake wa kushoto kwa njia ambayo ni Lionel Messi tu anaweza," alisema Nevin

Lakini kuna maswali kuhusu hatma ya Salah huko Anfield kwa kuwa Mumisri huyo bado hajasaini kandarasi mpya na aliyo nayo sasa inakamilika mwaka 2023.

Meneja wa Liverpool Klopp alisikia mwenye matumani wiki hii kuwa nyota wake atakubali mktaba mpya kitu ambacho mshambualiiji wa zamani Michael Owen anaamini kitafanyika.

Owen aliiambia BT Sport: "Mkataba wake utashughulikiwa, Lakini mambo ni magumu. Huu unaweza kuwa mkataba wake wa mwisho mkubwa katika taaluma yake kwa hivyo atachukua muda kufukiria.

" Anaweza kuenda wapi? Kandanda ya uhispania inakumbwa na changamoto.

Mlinzi wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand aliongeza: unafiki ameketi tu pale na ajenti wake akisema nendeni mumtafute mchezaji anayelipwa hela nyingi zaidi katika ligi na mumuongezee pauni kadhha juu yake? Ndiye mchezaji bora katika ligi kwa wakati huu.

Chanzo cha picha, Getty Images

'Singeweza kujivunia zaidi'

Wakati Liverpool, Atletico Madrid, Porto na AC Milan waliwekwa pamoja Agosti. Kundi B lilitajwa kuwa 'Kundi la Kifo' Lakini kikosi chake Klopp kilifagia timu zote kwa urahisi.

Kinakuwa kilabu cha kwanza cha Uingereza katika historia kushinda mechi zote sita kuu katika Champions League, wakifunga mara 17 na kufungwa bao sita.

Liverpool pia walishuhudia mechi sita za Champions League mfululizo kwa mara ya kwanza licha ya kufanya mabadiliko kadhaa katika kikosi cha kwanza wakimalizia ponti 11 mbele ya namba mbili.

"Nina furaha sana, alisema Klopp, hususan kwa mechi ya sita kwa kusema ukweli. Tulichagua kikosi kile sababu tulitaka kushinda mechi."

"Kile vijana walifanya, sitaweza kujivunia zaidi. Ilikuwa mechi nzuri, Nina furaha sana.