Omicron: Maswali yako matano kuhusu kirusi hatari cha corona yajibiwa .....

Chanzo cha picha, Getty Images
Mara tu omicron kilipotajwa kuwa aina ya kirusi kipya tarehe 26 Novemba, mjadala kuhusu kiruisi hiki ulichacha kwenye mitandao.
Kulingana na ripoti za Google zilizopatwa na BBC, omicron lilikuwa neno lililotafutwa sana kwenye mitandao.
Baada ya kugunduliwa nchini Afrika Kusini kurudi hiki tayati kimeripotiwa katika nchi 40 ikiwemo Argentina, Brazil, Chile, Mexico na Uhispania.
Kwa sasa, kwa uhakika haijulikani kina uwezo gani wa kuambukiza au ikwa kina uwezo wa kukwepa kinga iliyopatikana kutoka kwa chanjo ya maambukizi ya awali.
Utafiti uneandelea kufanywa kuelewa masuala haya na matokeo ya kwanza yanachapishwa mwezi huu.
Haya ni baadhi ya maswali maarufu mitandaoni na majibu kutoka kwa wataalamu
1. Omicron inamaanisha nini?
Omicrion ni herufi ya kumi na tano ya alfabeti za Kigiriki
Wakati aina za kwanza za kirusi cha corona kilianza kuonekana, wanasayansi walibuni mbinu ya kuviainisha
Ndipo SARS-CoV-2, kilichotambuaiwa kwanza Wuhan, China kilikuja kuwa kirusi aina ya A.
Baadaye wakati virusi zaidi zilipogunduliwa waligawana hizo namba ndiposa zikawa A.1, A.2, B.1.1, C.30.1, na kadhalika.
Lakini ilifika wakati mfumo huu ulisababisha kuchanganyikiwa wale wasio wataalamu katika nyanja hii.
Hii ndio moja ya sababu ilichangia shirika la afya duniani WHO kubuni mbinu Mei 2021 ya VOC, variant of concern ) na (VOI, variant of interest )
Kungana na alfabeti VOCs na VOls inamaanisha kuwa na mabadiliko muhimu yanayoweza kukifanya kirusi kusambaa kwa haraka kwa mafano.
Hivi ndivyo B.1.1.7, kilichogunduliwa nchini Uingereza kilikuja kuwa; B.1.351 (Afrika Kusini) kikawa beta; P.1 (Brazil) kikawa gamma; B.1.617.2 (India) kikawa delta; na B.1.1 .529 (Afrika Kusini) kikawa omicron.
Chanzo cha picha, Getty Images
Pia kuna sababua ya piliaya WHO kuamua kutumia alfabeti za kigiriki, sabanu ni kuzuia kile kirusi kuhusishwa na jina ambapo kiliibukia.
2. Kwa nini jina omicron?
Kuchaguliwa jina omicron kwa kirusi cha B.1.529 iliwapata jamii ya wanasayansi kwa mshangao.
Hii ni kwa sababu kirusi cha mwisho kupewa jina kwa alfabeti za Kigiriki kilikuwa ni VOI B.1.621, kilichogunduliwa nchini Colombia Janauri 2021. Kinajulikana kama mu, ambayo ni herufi namba 12 katika alfabeti ya Kigiriki.
Ndio ikafikiriwa kuwa jina ambalo litapewa kirusi ambacho kingefuata cha VOl au VOC litatakuwa herufi namba 13, ambayo ni nu.
Lakini WHO ikaamua kutoa herufi mbili zilizofuata na kutua kwa herufi ya 15: omicron.
Mtaalamu wa virusi Fernando Spilki kutoka chuo cha Feevale huko Rio Grande do Sul, Brazil anaeleza kuwa uamuzi huu unaweza kuhusu sauti ya herufi hizo katika baadhi ya lugha
"Ninajua watu waliohudhuria mikutano kuchagua jina hilo na moja ya sababu ya nu kuondolewa ni kuwa matamshi ya kiingereza huwa sawa na sauti new ['nuevo' kwa Kihispani]. Hilo laweza kuwachanganya watu wanaposkia neno hilo, hawawezi kujua kama ni kirusi kipya au kirusi cha nu" anaeleza.
3. Kipi kinafahamika kuhusu kirusi cha omicron?
Licha ya kugunduliwa hivi majuzi tu, omicron kilizua hisia nyingi kwa kuwa na mabadiliko kadhaa sehemu nyingi za kirusi cha corona.
"Aina hii ya kirusi kina mabadiliko makubwa, kitu mabacho hakikutarajiwa" anaeleza mtaalamu wa virusi Flavio da Fonseca, Profesa chuo cha Minas Gerais nchini Brazil.
Baadhi ya mabadiliko haya tayari yalifahamika kwetu kwa kuwa yalionekana pia kwa virusi vingine na yanachangia sana katika kusambaa sana kwa virusi ambavyo huambukiza zaidi na kupitishwa kwa haraka.
Chanzo cha picha, Getty Images
Kitu kingine muhimu ni uwezo wa omicron kutawala Afrika Kusini ni kimekuwa kirusi kinachoripotiwa zaid siku za hivi karibuni hata zaidi ya kile cha delta ambacha pia kiko kundi la VOCs.
Kwa hivyo wataalamu wanatajia maambukizi ya kirusi hiki kipya cha corona kuwa ya juu.
Lakini kuna mambao mengi ambayo hayana ufahamu, kama vile ni kwa kiwango gani omicron kinaweza akukwepa kinga iliyopatikana kupitia chanjo au baada ya maambukzi ya awali.
"Utafiti unafanyika kubaini athari kamili ya kirusi hiki katika matukio tofauti," anasema Spilki.
Chanzo cha picha, Getty Images
4. Kipi kinasabaisha kirusi cha omicron?
Licha ya mabadlikoa haya yote omicron bado ni SARS-CoV-2, ambacho ni kirusi kinachosababisha covid-19.
Jinsi inavyo fahamika vyema, kinasambaa kupitia matone ya mate au erosoli itokayo mdomo au pua la mtu aliyeambukizwa.
Mara nyingi uonjwa huu hauna dalili na mgonjwa hugundua baada ya muda. Lakini wengi wa walioambukizwa hukumbwa na usumbufu wenye nguvu na uhitaji kulazwa na wako katika hatari kubwa ya kufa.
Na hapo ni muhimu kujua kuwa njia za kujikinga zimebaki zile zile na omicron.
"Matumzi ya maski, kukaa mbali na mtu mwingine na chanjo bado hdizo hatua muhimu," anaeleza Fonseca.
5. Dalili za kirusi kipya cha omicron ni zipi?
Ripoti kutoka kwa madaktari waliomtibu mgonjwa wa kwanza nchini Afrika Kusini zinaonyesha mabadiliko muhimu kwenye dalili.
Dr . Angelique Coetzee anasema watu hawa mara nyingi hukumbwa na uchovu, uchungu kwenye misuli na kuwashwa koo, joto na kikohozi kavu.
Wakati wa mahojiano na BBC pia alisema kuwa wale walioambukizwa walionyesha athari nyepesi.
"Ilianza na mgonjwa aliye na dalili nyepesi. Alisema alikuwa na uchovu mwingi kwa siku mbili na alikuwa anaumwa na mwili na kichwa. Hakuwa akikohoa, hakupoteza harufu au ladha," alisema.
Chanzo cha picha, EPA
Wataalamu wanakushauri uwe makini na habari hii - unahitaji kusubiri zaidi kuwa na uhakika iwapo kirusi hiki kinasababisha dalili nyapesi.
"Habari zinazokuja kutoka Afrika Kusini za dalili nyapesi zinatupa matumaini lakini tunahitaji bado kuchunguza zaidi, anasema Fonseca.
"Bado tunahitaji kuelewa kuhusu omicron kitakuwa na tabia gani kwenye watu wa umri tofauti na baina ya makundi ya watu," anakubali Spikli.