Wanasayansi wanaoamini kuwa ulimwengu hauna mwanzo wake

,

Chanzo cha picha, Getty Images

Ikiwa watakuliza ulimwengu ulianzia wapi, Mshindo Mkuu au Bing Ban ndio jibu la wanza linaweza kuja akilini mwako.

Kuna wanasayansi hata hivyo wanaohoji iwapo huu ndio ulikuwa mwanzo.

Sasa mtafiti chipukizi anadai kuwa huenda hata hakukuwa na mwanzo wa ulimwengu.

Huyu ni Bruni Bento, mtafti katika idara ya sayansi ya hisabati katika chuo cha Liverpool nchini Uingereza.

Bento na mwandishi mweza wa jarida la "If Time Had No Beginning," ambalo kwa sasa linapitiwa na wataalamu wengine.

Nadharia yake inatofautiana na kile tunachokifahamu kuhusu kupita kwa nyakati, inaeleza kuwepo wakati uliopita usioisha na kuuona Mshindo Mkuu kama kisa kimoja zaidi katika ulimwengu ambacho kimekuwepo.

Pendekezo lake Bento ni lipi na linapinga kwa njia gani kile tunakijua kuhusu mwanzo wa ulimwengu?

Chanzo cha picha, Getty Images

Zaidi ya moja

Fisikia ya sasa ina nadharia mbili ambazo hutusaidia kuuelezea ulimwengu.

Kwa upande mmoja kipo kitu kijulikanacho kama quantum mechanics inayoelezea mwingiliano wa atomi na chembe

N kwa upande mwingine kuna kingine kujulikanacho kama general relativity kinachoeleza bayana mvuto unaoongoza kile kinachafanyika ulimwenguni.

Nadharia ya general relativity inaturudisha nyuma miaka bilioni 13.8 muda mfupi baada ya Mshindo Mkuu.

Nadhari hii ya Einstein hata hivyo ina kasoro ya kueleza kile kilitokea wakati ya Mshindi Mkuu au kipi kilifanyika kabla.

Hiki ndicho wataalamu wanakiita "umoja" na hapa ndipo nadharia ya relativity haielezi ni kipi kinafanyika.

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika nadharia hiyo ya umoja, vitu hubanwa na kuufanya mvuto kuwa wenye nguvu kubwa.

Kwa hivyo kinochohitajika kueleza kile kilifanyika wakati huo au kabla ni nadharia inayounganisha quantum mechanics na general relativity.

Nyakati za ulimwengu

Katika nakala yake Bento anatumia nadharia ya ni kipi kilichangia, nadharia inayoundwa na matofali ya kujenga atomi za nyakati.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kati hali hii mambo mengine yanasuluhisha tatizo la kitu kimoja kwa sababu kulingana na hili hakuna kitu kidogo kuliko atomi.

Hatuna mwanzo

Kazi ya Bento inaanzia suala hili kupendekeza kuwa mifumo iliundwa bila kikomo, kwa hivyo Mshindo Mkuu haukuwa mwazo wa ulimwengu.

Kwa Bento kawaida kuna kitu fulani kabla, kulikua na mifumo fulani hapo awali na mshido Mkuu ulikuja wakati fulani wa kukua kwa ulimwengu.

"Kazi yetu inasema ikiwa vianzo kadhaa ndio jibu, basi hatuna mwanzo," anasema Bento.

Chanzo cha picha, BAAC£NES

Kazi ya Bento inatoa hatua za kwanza za kuelezea hisabati ya Mshindo Mkubwa na uwezekano wake katika historia ya zamani.

Bento anaamini kuwa majaribio ya siku zijazo yanaweza kuwa ni matokeo ya kile anapendekeza.