Edouard Mendy: Jinsi kipa wa Senegal alivyokuwa nambari moja Afrika
- Na Victoire Eyoum
- BBC Sport Africa

Chanzo cha picha, Getty Images
Mendy alijisajili kama mtu asiye na ajira nchini Ufaransa 2014,lakini akawa mshindi wa Ligi ya Mabingwa miaka saba tu baadaye
Popote anapokwenda barani Afrika, Msenegal Edouard Mendy - kipa pekee wa Ligi Kuu England kutoka barani Afrika - anasema ametiwa moyo sana na wale anaokutana nao.
Nyota huyo wa Chelsea, 29, amekuwa na mwaka ambao hautawahi kusauhaulika tango alipojiunga na klabu hiyo Septemba 2020 kutokana na msisitizo wa mlinda mlango wa zamani wa klabu hiyo Petr Cech.
Sasa akijivunia melali za Champions League na Uefa Super Cup, Mendy ananza kuiga msururu wa ushindi wa mataji kama Czech -alipokuwa na the Blues - kupitia utendakazi usio na dosari.
"Inashangaza kwa sababu nimefanya watu wajivunie katika bara zima," aliambia BBC Sport Africa. "Kila mahali barani Afrika, ninapotembea barabarani, watu husimama kunipongeza.
"Ni kitu cha kipekee kwa sababu ukienda Afrika Kusini, Congo au Togo, halafu unapatana na watu hawa wote wanakwambia kuwa wanajivunia kuwa wewe, wanakuunga mkono na kukuambia uendelee na unachofanya.
"Hilo hunipa furaha kubwa na kunifanya nitake kuendelea kushinda."
Ushini ni kitu ambacho anaendelea kuzoea.
Msimu wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa ulikuwa wa ajabu - aliponyanyua taji, na kuwa kipa wa kwanza kutofungwa katika mechi (rekodi ya pamoja) katika mwaka wake wa kwanza na baadaye akatangazwa kuwa Kipa wa Uefa wa 2020-21.
"Ni shindano gumu zaidi Ulaya," alisema.
"Tulikuwa wazuri sana katika hatua ya makundi, hatua ya mtoano na fainali. Kwa mwaka wangu wa kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa, ilikuwa ni mechi nzuri ya kwanza."
Bao bora alilozuia 2021 pia lilikuwa katika shindano hilo, wakati alipomdhibiti Karim Benzema na Real Madrid katika mkondo wa pili wa nusu fainali ambapo Chelsea ilishinda mabao 2-0 na kujikatia tiketi ya fainali ya mwezi Mei dhidi ya Manchester City.
Huko Porto, Mendy alikua kipa wa kwanza Mwafrika kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa, hata kama Mzimbabwe Bruce Grobbelaar amefanya hivyo mara mbili katika mtangulizi wa dimba hilo, Kombe la Uropa (aliyeshinda 1984, lakini akapoteza 1985).
"Ni fahari kwangu na kwa familia yangu," alisema.
Grobbelaar na Mendy wanaunda nusu ya jumla ya makipa wa Ligi Kuu ya Afrika tangu ilipozinduliwa mwaka 1992, huku Mnigeria Carl Ikeme na Mghana Richard Kingson wakiwa wengine wa pekee.
"Najua ni jukumu na nimekuwa nikisema kila mara nitafanya kila niwezalo kuwafanya watu wajivunie na kuonyesha kunaweza kuwa na makipa wengi wa Kiafrika kwenye Ligi Kuu."
Mchezaji huyo anayejulikana kama 'Edou' katika klabu ya Chelsea anafanya hivyo - kwa kusajili mabao 36 katika mechi 65 za kwanza za Blues, na kutingwa mabao 42 pekee.
Kipa mwenza wa Cech
Mfahamu kipa wa Chelsea Edouard Mendy
Mendy anamshukuru Cech kwa kumsaidia kupata nafasi yake katika Ligi ya Premia. Safari ya Cech mwenyewe kutoka Rennes hadi Stamford Bridge ilisababisha ushindi mmoja wa Ligi ya Mabingwa na ubingwa mara nne miongoni mwa ushindi mwingine..
"Petr ilipambania sana usajili wangu kwa hivyo nilipowasili, Nilitaka sana kuwa mchezaji bora uwanjani - ili kumuonyesha amefanya chaguo bora zaidi," alisema Mendy.
Alianza vyema na aliazimia, kuendelea hivyo baada ya kutofungwa katika mechi sita ya kwanza kati saba, huku akiandikisha sare tasa katika mechi ya ugenini dhidi ya Manchester United - mechozo ambao bado anajivunia hadi wa leo.
"Nafikiria mechi dhidi ya Manchester United - moja ya mechi yangu ya kwanza kwenye Ligi ya Premia na Old Trafford, ambayo inajulikana sana katika kandanda kama moja ya sehemu nzuri zaidi za kucheza."
Mendy anasema aliweza kupiga hatua nchini Uingereza kwa sababu tayari alijua na "kuipenda" nchi hiyo, kwani aliwahi kumtembelea dadake yake aliyekuwa akiishi nchini humo.
Alipoulizwa kuhusu mabadiliko makubwa ambayo alipaswa kuzoea, Mendy alielezea kiwango cha kasi katika ligi kuu ya Uingereza na ratiba yake ya Krismasi iliyojaa hadi pomoni.
Uchochole hadi utajiri
Wakati akitafakari juu ya kuinuka kwake, Mendy anamshukuru baba yake na kaka yake kwa kumwezesha kushinda changamoto kubwa.
"Baba yangu alinihusia kufanya kazi kwa bidii ikiwa nataka kufanikiwa maishani, huku kaka yangu akinipeleka uwanjani kufanya mazoezi, kwa hivyo ni familia yangu imesimama na mimi na kuniunga mkono na kunisukuma kufikia malengo yangu."
Ingawa alitia saini kandarasi yake ya kwanza ya kulipwa mwaka 2011 na timu ya daraja la tatu Cherbourg ya Ufaransa, ambako alikulia, aliingia kwenye jangwa la soka mkataba huo ulipokamilika mwaka 2014.
Baada ya kupotoshwa na wakala, alikaa mwaka mmoja bila klabu na hivyo kukosa mapato. Mchezaji huyo ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 22 alilazimika kujisajili katika shirika la wasio na ajira la Ufaransa huku akifikiria kwa uzito mustakabali wake.
Chanzo cha picha, Getty Images
Edouard Mendy na Chelsea wanasherehekea ushindi wao wa Ligi ya Mabingwa 2021
Lakini baada ya mchezaji mwenza wa zamani kumpendekeza Mendy kwa rafiki yake huko Marseille, Msenegali huyo alijiunga kama kipa chaguo la nne kabla ya uchezaji wake wa wachezaji wa akiba kumkuta akivutiwa na mahali pengine.
Mendy alichagua timu ya Ligue 2, Reims, ambayo aliisaidia kushinda kupandishwa cheo, na baada ya msimu wa kwanza mzuri kwenye ligi ya daraja la kwanza ya Ufaransa akapata motisha ya kuhamia Rennes 2019, kiwango chake kizuri cha uchezaji kiligunduliwa na Chelsea iliyotumia pesa nyingi kumwinda Mendy ambaye wakati mmoja alikuwa uhaba wa pesa.
"Hadithi yangu inaweza kuashiria matumaini kwa watu wengi, kwa sababu kuna wachezaji wengi vijana ambao wanaweza kujikuta katika hali yangu," anasema.
"Ni mchanganyiko wa imani , uvumilivu na bidii- kwa sana. Unahitaji kujiamini na wakati wote kuongeza juhudi kuliko wengine."
Umahiri wa Mendy uwanjani umemfanya atunukiwe tuzo ya mchezaji soka wa mwaka wa Senegal na hivyo basi kuhitimisha msururu wa mataji sita mfululizo ya Sadio Mane wa Liverpool.
Mwezi uliopita, pia alitambuliwa kama mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani - mshindi wa pili katika taji la Yashin Trophy, ambalo hutolewa kwa kipa bora zaidi barani Ulaya na Soka ya Ufaransa wakati wa dhifa ya tuzo ya Ballon d'Or.
"Miaka michache iliyopita, sikuwa na kazi, wala klabu, na leo natajwa kuwa miongoni mwa makipa bora zaidi duniani. Inanionyesha nkuwa nipo kwenye njia sahihi, na nipo sehemu sahihi ya kuchukua mataji na kuwa bora zaidi." Duniani.
Tafadhali Mpigie kura Mwanamichezo Bora wa Afrika wa BBC 2021 ambapo pia utapata sheria na ilani ya faragha. Upigaji kura utafungwa Jumapili Disemba 19 2021 saa 23:59 GMT."