Chombo cha Parker chaweka historia kwa kupita anga ya jua

Artwork: Parker Solar Probe

Chanzo cha picha, NASA-JHU-APL

Maelezo ya picha,

Parker lazima kila wakati aweke ngao yake ya joto ikielekezwa kwenye Jua, jinsi mchoro huu unavyoonyesha

Shirika la anga za mbali la Marekani (Nasa) limeitaja kuwa historia - mara ya kwanza kwa chombo cha anga za mbali kupita katika anga ya nje ya jua.

Kiwango hicho kiliafikiwa na chombo cha Parker Solar Probe, kilichovuka kwa muda mfupi kwenda eneo linalozunguka nyota yetu ambalo wanasayasi wanaliita corona.

Hilo lilitokea mwezi Aprili na utafiti kwenye data umethibitisha kwa sasa.

Chombo cha Parker kilistahilimIli joto kali na mionzi lakini kilikusanya taarifa mpya kuhusu vile jua linafanya kazi.

"Kama vile kutua mwezini kuliwasaidia wanasayansi kuelewa jinsi ulivyoundwa, kugusa mwezi ni hatua kubwa kwa mwanadamu kutusaidia kupata habari muhimu kuhusu nyota iliyo karibu nasi," alisema Nicola Fox mkuu wa kitengo cha heliophysics shirika la Nasa.

Chombo hiki kilichozinduliwa miaka mitatu iliyopita, lengo lake ni kufanya safari zai za kurudia za karibu na jua.

Chombo hicho kinasonga kwa mwendo wa kasi kubwa ya zaidi ya kilomita 500,000 kwa saa. Lengo ni kuingia kwa haraka na kutoka kwa haraka kikifanya vipimo kuhusu mazingira kwa kutumia vifaa vilivyo nyuma ya ngao nene ya kuzuia joto.

Chanzo cha picha, S R Habbal and M Druckmüller

Maelezo ya picha,

Corona iliyoenea inaonekana kwetu tu Duniani wakati wa kupatwa kamili kwa jua

Tarehe 28 mwezi huu, Parker kilivuka mpaka unaojulikana kama Alfvén. Hii ni sehemu ya nje ya corona.

Parker kilifika mpaka wa karibu kilomita milioni 13 kutoka kwa jua.

Data za chombo hicho zinaonyesha kuwa kilizunguka mara tatu kwa muda wa saa tano kulingana na Stuart Bale kutoka chuo cha California.

Watafiti wanavutiwa na corona kwa sababu ndipo mambo muhimu hufanyika ambayo kwa sasa yanapingana na maelezo.

Moja ni kile kinaonekana kuwa joto la juu. Viwango vya joto vya jua vipo kwenye kile tunoana ni nyusi 6,000 lakini kwenye corona vinaweza kuwa mamilioni ya nyusi au zaidi.

Ni katika eneo hili ambapo mtiririko wa nje wa chembe zenye kasi ghafla hubadilika kuwa upepo wenye kasi ya supersonic suala ambalo pia ni fumbo.

Kikosi cha wanasayansi wa Parker kitakusanya data zaidi wakati chombo hicho kinachunguza ndani zaidi ya corona. Kinatarajiwa kufika ukaribu kwa kilomita milioni 7 karibu na jua ifikapo mwaka 2025.

Miale mikubwa ya jua inaweza kuvuruga mvuto wa dunia yetu. Katika hali hiyo mawasiliano yanaweza kuvurugwa, setilati zinaweza kutupwa nje wa njia zao na lainicxd87 za umeme zinaweza kukumbwa na hitilafu.

Wanasayansi wanajaribu kutabiri masuala haya na Parker kinaahidi kuwapa habari mpya kusaidia kufanya hivyo.