10 wafa katika maporomoko Kenya

Watu kumi wamethibitishwa kufa na wengine 15 hawajulikani walipo kufuatia maporomoko ya udongo katika wilaya ya Marakwet, magharibi mwa Kenya.

Image caption Maporomoko ya udongo Brazil. Hali kama hiyo imetokea Kenya.

Maporomoko hayo yametokea alfajiri ya Ijumaa. Idadi kubwa ya waliokufa ni watoto. Wakazi wa huko wanasema maporomoko hayo yametokea baada ya mvua kubwa kunyesha.

Miili ya watoto wenye umri wa miaka 10 hadi mitatu iliyosombwa na maji imepatikana kwenye mto katika eneo hilo.

Shughuli za uokoaji zinafanyika katika eneo hilo lenye milima.

watu saba wamejeruhiwa katika tukio hilo na wamepelekwa hospitali.

Shirika la misaada la Red Cross na kitengo cha kukabiliana na majanga cha serikali ndio wanaongoza shughuli hiyo.

Marakwet ipo katika eneo karibu na bonde la ufa, na wakazi wa eneo la tukio wanaishi karibu na mto.