Mswada kukataza wake wengi wapingwa Malawi

Raia wa Malawi
Image caption Raia wa Malawi

Mswada wa sheria unaopendekeza kupiga marufuku wanaume kuwa na zaidi ya mke mmoja, umezua hisia kali nchini Malawi, hasa kutoka kwa jamii ya kiislamu.

Msemaji wa Baraza la Waislamu nchini humo, Imran Shareef Muhammed, ameiambia BBC kuwa sheria hiyo itawabagua waumini wa dini hiyo.

Amesema idadi ya wanawake nchini humo ni kubwa kuliko ile ya wanaume kwa asilimia 6 na ikiwa sheria hiyo itapishwa, idadi kubwa ya kina mama hawataolewa.

Ameongeza kuwa hatua kama hiyo inaweza kusababisha kuongezeka kwa idadi ya kina mama wanaojihusisha na ukahaba ili kukithi hali ya masiha.

Waziri wa masuala ya jinsia nchini humo, hapo jana alisema, sheria hiyo itazuia dhuluma dhidi ya kina mama katika ndoa kama hizo.