Mshukiwa wa shambulizi akamatwa Marekani

Raia wa Marekani mwenye asili ya kigeni amekamatwa kwa kuhusika na jaribio lililotibuka la shambulizi la bomu iliyotegwa ndani ya gari mjini New York hapo Jumamosi.

Mkuu wa sheria , Erick Holder amesema mwanamme huyo, Faisal Shazad alikamatwa katika uwanja wa ndege wa John F kennedy Mjini New York wakati akijaribu kuondoka nchini kuelekea Dubai.

Faisal Shazad, Alizaliwa nchini Pakistan lakini akapata uraia wa Marekani. Akitoa taarifa hiyo, Mwanasherua mkuu wa Marekani Erick Holden amesema vyombo vya usalama vilikusanya ushahidi uliosaidia kukamatwa kwa Shazad.

Aidha alisema uchunguzi zaidi unandelea kufuatia jaribio hilo la shambulizi la bomu.

Bw. Holder amesema pia kuwa shambulizi hilo lililenga kuwaua raia wa Marekani. Hapo jumamosi gari moja lilipatikana likiwa na mabomu katika eneo la Times Square mjini New York.

Maafisa wa usalama walifaulu kuyategua mabomu hayo kabla ya kulipuka.Faisal Sahzad atafikishwa katika mahakama ya Manhattan baadaye leo. Hata hivyo mashataka dhidi yake hayajatolewa.