Wanamgambo Somalia washambulia hospitali

Somali militants
Image caption Wanamgambo wa Kiislamu mjini Mogadishu

Wanamgambo wa Hisbul- ul-Islam nchini Somalia wameshambulia hospitali moja nje ya mji mkuu Mogadishu. Shambulio hilo limeelezewa kuwa la kulipiza kisasi kufuatia mauaji ya kamanda mmoja wa kundi hilo.

Wanamgambo hao wameshtumu walinzi wa hospitali hiyo kwa kutekeleza mauaji hayo. Hatahivyo madaktari wa hospitali hiyo wanasema hawakujua lolote.

Mtu mmoja ameripotiwa kujeruhiwa katika shambulio hilo ambalo limetatiza shugli katika hospitali hiyo ambayo huwapa chakula watoto wenye utapiamlo wanaoishi katika kambi iliyopo kando ya barabara ya kutoka Mogadishu kuelekea Afgoye.

Image caption Somalia ni moja wapo ya nchi hatari zaidi kufanya kazi za uandishi wa habari

Wakati huohuo watu wenye silaha wamuua mwanahabari maarufu nchini Somalia aliyekuwa akifanya kazi katika radio ya taifa mjini Mogadishu.

Sheikh Nur Abkey alitekwa nyara hapo Jumanne na mwili wake ukapatikana umetupwa baadaye jioni hiyo.

Bado haijabainika wazi ni nani aliyemuua lakini wanahabari wenzake wanasema aliuawa kwasababu alikuwa mfanyikazi wa radio Mogadishu ambayo hukosoa vikali mienendo ya wanamgambo wa Kiislamu.