Mipango ya kombe la dunia imekamilika

Kombe la Dunia limewasilishwa Afrika Kusini

Imesalia majuma kadhaa kabla ya kuanza fainali za kombe la dunia. Maafisa Afrika Kusini wamesema viwanja vyote kumi vitakavyoandaliwa fainali hizo viko tayari.

Tayari kombe linaloshindaniwa limewasilishwa Afrika Kusini ambako limekuwa likizunguzhwa katika maeneo kadhaa huku maelfu ya raia wakijitokeza kilikaribisha.

Viwanja vitano vipya vimejengwa huku sita vikikarabatiwa.

Aidha tikiti zote ziko karibu kumalizika.Hata hivyo huenda idadi ya wageni waliotarajiwa kuwasili nchini humo ikapungua kutokana na msukosuko wa kiuchumi unaokumba dunia.

Mwandishi wa BBC Mjini Johannesburg amesema raia wa Afrika Kusini wamenunua tikiti zilizosalia.

Huku haya yakiarifiwa shirikisho la soka duniani {FIFA} limekiri kumimina dola milioni 100 katika maandalizi ya kombe la dunia mwaka huu Afrika Kusini kuhakikisha mipango yote inakamilika.

Katibu Mkuu wa Fifa Jerome Valcke ameambia BBC kwamba shirikisho hilo lilisaini asili mia 25 zaidi ya fedha wakati wa kikao cha baraza kuu mwezi Machi.

Fedha hizo zilinuia kuimarisha kambi za mazoezi zitakazotumika na timu tofauti.