Rais wa Sudan Kusini aapishwa

Salva Kiir
Image caption Salva Kiir

Salva Kiir, aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi la SPLM kusini mwa Sudan, ameapishwa kuwa Rais wa kwanza kuchaguliwa katika eneo linalojitawala lenyewe kusini mwa nchi hiyo.

Kuapishwa huko kunafuatia ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi wa mwezi Aprili, ambapo ni sehemu ya makubaliano ya amani yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 21 baina ya upande wa kaskazini na kusini.

Mwakani, watu wa upande wa kusini mwa Sudan watapiga kura kuamua iwapo itawezekana wawe huru kabisa.

Mwandishi wa BBC aliyopo Juba amesema inaaminika kuwa wakipewa nafasi ya kupiga kura, basi wengi watataka eneo hilo liwe huru.

Kiwango kikubwa cha mafuta kipo upande wa kusini, na mpaka kamili baina ya pande hizo mbili bado unahitaji kutambuliwa.