Ufaransa yaandaa kongamano na Afrika

Nicholas Sarkozy anakutana na viongozi wa Afrika

Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy anafungua kongamano kati ya Ufaransa na nchi za Afrika katika mji wa Nice baadaye leo.

Kati ya mataifa 53 ya afrika ni nchi mbili pekee ambazo zimekosa kutuma wajumbe wake.

Nchi ya Madagascar haikualikwa kwenye kongamano hilo huku Zimbabwe ikikataa kutuma uwakilishi baada ya Ufaransa kupinga kuwepo kwa rais Robert Mugabe.

Makundi ya kutetea haki za binadamu chini ya mwavuli wa "Civil Liberties" yamekosoa kongamano hilo yakisema viongozi 38 kutoka Afrika wanaoshiriki mkutano huo wamelaumiwa kwa kuhusika na ukiukaji wa haki za binadamu.

Kongamano hilo litaangazia ushirikiano wa kibiashara kati ya Ufaransa na Afrika,uharamia, vita dhidi ya ugaidi na mabadiliko ya hali ya hewa.