Boti ya abiria yahofiwa kuzama Liberia

Ufuo wa Bahari nchini Liberia
Image caption Ufuo wa Bahari nchini Liberia

Maafisa wa serikali ya Liberia, wamesema mashua moja ambayo inakisiwa kubeba zaidi ya abiria 100 imetoweka.

Helicopta mbili zimetumwa katika eneo la tukio ili kusaidia katika shughuli ya kuitafuta mashua hiyo kwa ushirikiano na wavuvi wa eneo hilo.

Meneja mmoja katika bandari ya mji wa Kusini wa Harper, amesema walipokea mawasiliano ya mwisho kutoka kwa boti hiyo jana jioni.

Boti hiyo ilikuwa ikielekea mji wa Maryland, ulioko Kusini Mashariki mwa nchi hiyo kutoka mji mkuu wa Monrovia.