Raia kutoa maoni kuhusu katiba:Nigeria

Watu waliouawa kwenye ghasia nchini Nigeria
Image caption Watu waliouawa kwenye ghasia nchini Nigeria

Wabunge wa Nigeria leo wataanza kupokea maoni na mapendekezo ya umma kuhusu mabadiliko ya katiba kama juhudi zao za kutaka kurekebisha katiba ya nchi.

Wale watakaotaka kutoa maoani yao, watakusanyika katika majengo ya bunge mjini Abuja. Kumekuwepo na madai kuwa uchaguzi wa mwaka 2007 na ule wa 2003 ulikumbwa na wizi wa kura na udanganyifu.

Juhudi hizi zinafanyika huku uchaguzi mkuu nchini humo ukitarajiwa mapema mwaka ujao.

Rais wa sasa wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza kuwa atamteua mkuu mpya wa tume ya uchaguzi baadaye wiki hii, ingawa wanharakati wa demokrasia wanapinga rais kuwa na mamlaka ya kumteua mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi.