Madaktari wagoma nchini Nigeria

Raia wa Nigeria
Image caption Raia wa Nigeria

Madaktari wa vyeo vya chini nchini Nigeria, wameanza mgomo wa siku tatu, kulalamikia mishahara ndogo wanayopata na hali duni ya utendaji kazi.

Madaktari hao wanadai kuwa mafunzo yanayotolewa na taasisi za matibabu nchini humo ni ya chini zaidi na kwamba serikali ya nchi hiyo haina nia ya kutatua tatizo hilo.

Chama cha madaktari nchini Nigeria, kinawakilisha madaktari wa vyeo vya juu pekee na kimetangaza kuwa hakitashiriki kwenye mgomo huo.