Rio Ferdinand nje ya timu ya England

Rio Ferdinand akiwa anatembelea gongo
Image caption Rio Ferdinand akiwa anatembelea gongo

Nahodha wa England Rio Ferdinand atakosa Kombe la Dunia baada ya kuumia goti katika mazoezi ya mwanzo nchini Afrika Kusini.

Ferdinand amepumzishwa kwa takriban wiki nne mpaka sita ikiwa kano ya goti lake la kushoto limepata jeraha.

Mlinzi wa klabu ya Tottenham Michael Dawson atasafiri siku ya Ijumaa kuziba nafasi ya Ferdinand, huku Steven Gerrard akichukua nafasi yake ya nahodha.