NATO yashambuliwa Pakistan, 7 wauawa

Image caption Magari ya NATO yachomwa Pakistan

Wapiganaji wameshambulia kwa risasi msafara wa vikosi vya kujihami vya nchi za magharibi NATO karibu na mji mkuu wa Pakistan,Islamabad.

Waliwaua watu saba na kuchoma moto magari kadhaa kabla ya kutoroka. Polisi wamesema kuwa zaidi ya watu 12 walihusika wakiwa wamejihami kwa magruneti na vilipuzi vingine. Shambulio hilo lilitokea 10KM kutoka mji huo wa Islamabad.

Mwandishi wa BBC mjini humo amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa shambulio kama hilo kutokea karibu sana na mji mkuu.

Image caption Magari ya NATO yachomwa Pakistan

Magari hayo ya NATO yalikuwa yanasafirisha bidhaa kwa wanajeshi wao nchini Afghansitan.