Afrika Mashariki kusoma bajeti zao leo

Hii leo mataifa manne wanachama wa Afrika Mashariki yatasoma makadirio yao ya fedha ya mwaka 2010 na 2011.

Mawaziri wa fedha wa Rwanda, Tanzania,Uganda na Kenya watawasilisha bajeti kwa mabunge ya nchi yao.

Burundi pekee imeachwa nje katika shughuli muhimu ya leo huko Afrika Mashariki.

Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa taifa hilo kutosoma bajeti yake sanjari na mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Maafisa wa serikali wanasema kuwa japo wanaelewa umuhimu wa kusoma bajeti yao pamoja na wenzao wa jumuiya ya Afrika mashariki, bado kuna masuala ya kiufundi kama vile marekebisho ya katiba ya nchi ambayo yanakuwa kikwazo kikubwa kwao.

Burundi itasoma bajeti yake mwishoni mwa mwaka.