Watu 2 wauawa kwenye msongamano-Ivory Coast

Alpha Blondy
Image caption Alpha Blondy

Takriban watu wawili wamefariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa vibaya kufuatia msongamano wa watu wakati wa tamasha ya muziki iliyoongozwa na msanii wa mtindo wa Raggae Alpha Blondy, katika uwanja mmoja wa michezo nchini Ivory Coast.

Ripoti zinasema tukio hilo lilitokea mjini Bouke wakati umati mkubwa ulipokuwa ukijaribu kuingia uwanja huo muda mfupi tu baada ya tamasha hiyo kuanza.

Mwanamuziki huyo, yuko katika ziara rasmi nchini humo nyenye maudhui amani na urafiki.