Ghana yaanza vyema

Asamoah Gyan
Image caption Asamoah Gyan

Ghana imekuwa na mwanzo mzuri kwenye kombe la dunia baada ya kuifunga Serbia bao 1-0 katika kundi la D.

Asamoah Gyan ndiye aliyefunga bao la Ghana kupitia mwaju wa penalti katika dakika ya 85.

Penalti hiyo ilipatikana baada ya Zdravko Kuzmanovic kuunawa mpira akijaribu kuondosha hatari ya shambulizi la Ghana.

Mara mbili Gyan alipata fursa ya kufunga lakini mpira ukagonga besela.

Serbia walimaliza wakiwa wachezaji 10 baada ya mlinzi Aleksandar Lukovic kupewa kadi nyekundu kutokana na mchezo mbaya kunako dakika ya 74.

Ushindi wa Ghana ni wa kwanza kwa timu za Afrika, baada ya Afrika Kusini kutoka sare 1-1 na Mexico, Algeria kufungwa 1-0 na Slovenia, nao Nigeria kufungwa 1-0 na Argentina.

Timu zingine katika kundi hilo la D ni Ujerumani na Australia.