5 wauawa katika mplipuko mjini Nairobi

Nchini Kenya, Watu 5 wamethibitishwa kufa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa baada ya milipuko iliyotokea jana katika mkutano wa kupinga katiba mpya inayopendekezwa.

Mkutano huo ulikuwa umepangwa na viongozi wa kidini Mjini Nairobi na ulihudhuriwa na maelfu ya watu wakiwemo wanasiasa. Polisi wanasema uchunguzi unaendelea na bado hawajui kilichosababisha milipuko hiyo japo huenda ikawa bomu ya kujitengenezea nyumbani.

Uchunguzi bado unaendelea kujua ni nani waliohusuka. Hata hivyo tayari makundi hasimu yameanza kuelekezeana lawama. Kundi la "NO" linalopinga katiba hiyo linadai kuwa huenda mlipuzi huyo alilenga kuhujumu mkutano wao na kulaumu polisi kwa kutotoa ulinzi wa kutosha kwao.

Waziri mkuu Raia Odinga hata hivyo amepuuza lawama hizo akisema kuwa kulikuwa na ulinzi wa kutosha. " Tusihusishwe na milipuko hiyo kwani sisi kama serikali hatuwezi kuruhusu raia waangamizwe. Kwani sio sisi tuliotoa kibali cha kufanyika mkutano huo?" aliongeza Raila.

Wakati huo huo, polisi wamegundua maiti ya mtu mmoja ndani ya gari aina ya Prado, aliyepigwa risasi na kuuawa mahali pa milipuko hiyo. Haijulikani iwapo kisa hiki kina uhusinao wowote na milipuko ya awali na tayari uchunguzi umeanzishwa.