Waziri wa fedha atoa ahadi ya mabadiliko

Waasi nchini Nigeria
Image caption Waasi nchini Nigeria

Waziri mpya wa Fedha wa Nigeria, Dkt. Olusegun Aganga, ameiambaia BBC kuwa taifa hilo linapaswa kuimarisha uchumi wake ili isitegemea mapato ya mafuta pekee.

Dkt. Aganga amesema kuwepo kwa mafuta nchini Nigeria kulikuwa baraka, lakini sasa imegeuka na kuwa laana.

Nigeria ndio nchi ya kumi duniani kwa uzalishaji wa mafuta, lakini eneo la Niger Delta ambalo lina utajiri mkubwa wa rasilimali hiyo imekubwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi kadhaa ya waasi.

Waasi hao wanadai kuwa eneo lao linatoa kiasi kikubwa cha mapato ya serikali lakini wao hawapati chochote kutokana na mauzo ya mafuta hayo.

Secta zingine za uchumi kama vile kilimo na viwanda zimeshindwa kuimarika kwa sababu serikali ya nchi hiyo inashughulikia kwa hali na mali secta ya mafuta pekee.

Bwana Aganga amesema atajirbu kuimarisha secta ya kawi na pia kuhimiza uwekezaji katika secta ya kilimo.