Wafuasi wa Rwasa wazuia polisi kumkamata

Agathon Rwasa
Image caption Agathon Rwasa

Mamia ya wafuasi wa upinzani wamepiga kambi usiku kucha katika nyumba ya mwanasiasa wa chama cha upinzani cha FNL, Agathon Rwasa, kuzuia polisi kumtia nguvuni.

Hii inafuatia kutolewa kibali cha kukamatwa kwake kutoka kwa idara ya polisi, kwa madai kuwa alitoa matamshi ya uchochezi mjini humo.

Rwasa pia ametajwa kuhusika na milipuko ya gruneti iliyotokea mjini Bujumbura mwishoni mwa wiki iliyopita.

Serikali ya Burundi bado haijatoa taarifa zozote kuhusu mashambulizi hayo ya guruneti ambayo yalitokea mwisho juma mjini Bujumbura.

Hata hivyo Rwasa anadai kuwa anaandamwa na serikali kwa lengo la kumhujumu kisiasa.