Mshukiwa wa shambulizi akiri makosa Marekani

Image caption Mshukiwa wa njama ya kulipua bomu katika eneo la Times Square nchini Marekani

Mtu anayedaiwa kupanga njama ya kulipua bomu lililotegwa ndani ya gari katika bustani la Times Square mjini New York Marekani, mwezi May, amekiri mashtaka yote kumi dhidi yake.

Faisal Shahzad raia wa Pakistan, amekiri kumiliki zana zenye maangamizi makubwa akiwa na nia ya kutumia katika njama yake iliyotibuka.

Shahzad aliyekamatwa siku mbili baada ya shambulizi hilo wakati akijaribu kuondoka nchini humo kuelekea Dubai, alikiri kugeza gari lake lililokuwa na bomu karibu na eneo la Times Square jumamosi jioni.

Bomu hilo lilipatikana baadaye huku stakabadhi za mahakamani zikidai kuwa bwan Shazhad alipokea pesa pamoja na mafunzo kuhusu namna ya kulipua mabomu kutoka kwa kundi la Taleban nchini Pakistan.

hata hivyo alisema yuko tayari kukiri makosa hayo kuonyesha kuwa Marekani ingali inakabiliwa na tisho la mashambulizi zaidi ikiwa hawatondoka nchini Afghanistan na Iraq.