England yasonga mbele

Image caption Defoe ndiye aliyeiokoa England ilipochuana na Slovenia

England imefufua ndoto yao katika Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, baada ya kuifunga Slovenia bao 1-0 na hivyo kufuzu kwa raundi ya pili.

Bao hilo la ushindi la England lilifungwa na Jermain Defoe katika kipindi cha kwanza.

Ushindi huo ulipokelewa kwa furaha kubwa kote nchini Uingereza ambako shule nyingi na biashara zilifanya maandalizi maalum ili watu waweze kutazama mchuano huo muhimu.

Katika mchuano mwingine wa kundi hilo la C, Marekani ilipata bao katika muda wa ziada na kuishinda Algeria bao 1-0, na pia kufuzu kwa raundi ya pili.

Algeria imekuwa timu ya tatu kutoka Afrika kuondolewa kwenye michuano hiyo.