Paraguay yaishinda Japan kwa penalti

Paraguay dhidi ya Japan
Image caption Paraguay iliishinda Japan kwa penalti tano kwa tatu

Paraguay imeshinda pambano la kwanza kwa mikwaju ya penalti katika michuano ya Kombe la Dunia ya 2010 na kufaulu kuingia robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia yake ambapo watacheza na mshindi kati ya Hispania na Ureno.

Paraguay ilifunga mikwaju yake yote mitano baada ya pambano lake na Japan kumalizika bila ya kufungana mwishoni mwa muda wa ziada.

Pambano hilo lilikosa msisimko wakati kila upande ukijidhatiti kulinda lango lao.

Matumaini ya Japan yalitoweka baada ya Yuichi Komano kugonga mwamba.

Paraguay iliibuka na ushindi wa penalti tano kwa tatu.

Kushindwa kwa Japan kulimaanisha bara la Asia halitakuwa na mwakilishi katika duru ya robo fainali.